Kada wa Chama Cha Mapinduzi , Methusela Gwajima |
Methusela Gwajima (kushoto) akitoa tamko, Pius Yalula (kulia) Afisa habari idara ya Maelezo. |
Wanahabri wakifuatilia tukio hilo.
KAKA wa Askofu wa kanisa la Ufufuo na Uzima, Josephat Gwajima aitwaye
Methusela Gwajima amemtaka mdogo wake kwenda kumuomba radhi Askofu Mkuu
wa Jimbo Katoliki Dar es Salaam Mhadhama Polycarp Kadinali Pengo kwa
kutoa lugha ya kumkashifu.
Akizungumza na wanahabari leo Jijini Dar es Salaam, Methusela alisema
ameamua kutokufumbia macho kitendo cha ndugu yake kumkashifu Pengo na
kwamba anapaswa kujitathimini alipopotoka kwa kumtukana kiongozi mkubwa
wa kiroho kwani ni sawa na kuidhalilisha familia nzima ya Ukoo wa
Gwajima.
Alisema maneno yake ya kashfa ni dhahiri ya kuwa hata ukoo mzima
umedhalilishwa hivyo familia ya Methusela Gwajima imemtaka kuomba
radhi mara moja.
Hata hivyo alisema kuwa yeye ni kada wa CCM hivyo amepata usumbufu
mkubwa tokea sakata hilo liibuke maana ndugu na marafiki walioko nje ya
nchi wamekuwa wakimuuliza kuhusiana na suala hilo hali inayompa wakati
mgumu kuwapatia majibu.
Alisema kashfa hizo hazina tija kwa taifa na haileti uhusiano mwema
baina ya madhehebu ya dini, bali yanachochea chuki, uhasama, utengano
na hasira kati ya wakristo kwa wakristo.
PICHA/STORINA DENIS MTIMA/GPL
|
No comments:
Post a Comment