Bidhaa
zinazoingizwa nchini:
Kuhusu bidhaa zinazoingizwa nchini,
anasema kwamba wakala wake unakagua vipimo vya bidhaa hizo kwa mujibu wa sheria
ya nchi na kuhakisha kwamba muagizaji anaingiza nchini bidhaa kama
ilivyokusudiwa.
“Kwa mfano mfanyabishara anayeagiza
viberiti hana budi kuingiza nchini viberiti vyenye idadi ya njiti inayokubalika
kisheria kisheria ,” anasema na kuongeza kwamba katika hilo wakala wake
hauna maskhara kwani wanahesabu hadi idadi ya njiti za kiberiti lengo likiwa ni
kumlinda mtumiaji wa mwisho ambaye ni mwananchi.
“Mfanyabiashara anapoagiza mfano
sabuni za kuogea, tuhahakikisha kwamba vipimo vya sabuni hiyo viko sahihi
na kwamba uzito wake uko sawa, tukigundua kuwa kuna mapungufu basi kuna sheria
na kanuni ambazo zinatuongoza katika kuchukua hatua,stahiki,” anasema.
No comments:
Post a Comment