Mkurugenzi wa Masoko na Uhusiano wa UTT-AMIS, Daud Mbaga akizungumza katika moja hafla za taasisi hiyo |
Swali: Ni fursa
gani nyingine Mtanzania anazipata kwa Uwekezaji huu wa vipande unaofanywa na UTT-AMIS?
Jibu:Fursa ya kwanza kubwa ni kwamba
mwekezaji anafaidika na ukuaji wa fedha zake na gawio la fedha kwa wale
waliowekeza katika mfuko ambao hutoa
gawio. Vilevile mwekezaji anakuwa amejiwekea akiba ya fedha zake ili aweze kufanya
uwekezaji anaohitaji. Lakini vipande pia vinaweza kutumika kama dhamana na
kumuwezesha mwekezaji kapata mkopo kutoka katika taasisi za kifedha kwa wale
watakao hitaji kufanya hivyo. Pia kuna mfuko kama Mfuko wa Wekeza Maisha ambao
unatoa faida pacha za kukuza mtaji na faida za bima.Katika mfuko huo wawekezaji
hunufaika kwa bima za maisha,ulemavu wa kudumu na ajali kwa gharama nafuu sana
ambapo ni vigumu kupata katika masoko ya kawaida ya bima. Vilevile inawapa
fursa ya watanzania wengi zaidi kushiriki katika uwekezaji katika masoko ya
fedha na mitaji.
No comments:
Post a Comment