Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Jakaya Kikwete akizungumza
na Afisa Mtendaji mkuu wa Wakala wa Vipimo Bi. Magdalena Chuwa
alipotembelea banda la Wizara ya Viwanda na Biashara kwenye kilele cha
maadhimisho ya siku ya Wanawake Duniani hivi karibuni
Katika sehemu ya Makala hii kwa wiki iliyopita tulijifunza namna serikali kupitia WMA inavyokabiliana na tatizo la vipimo batili maarufu kama Lumbesa, leo Afisa Mtendaji Mkuu wa WMA Magdalena Chuwa anazungumzia Vipimo
katika Sekta Gesi hapa nchini,fuatana naye uelimike zaidi.
Katika kipindi cha uongozi wa
serikali ya awamu ya nne,Wakala umeandaa kanuni ili kuhakikisha kwamba watumiaji wa gesi wa
majumbani, watumiaji wa viwandani na wasambazaji (wazalishaji), wote wanatumia
vipimo sahihi kwa mujibu wa sheria za nchi,ili Tanzania iweze kunufaika na
rasilimali hii muhimu katika uchumi wake.
Anasema kwamba kwa kuwa katika nchi
yetu imegundulika hazina kubwa ya gesi hivyo ni dhahiri kwamba matumizi ya gesi
kwa ujumla katika nchi yetu yameongezeka sana hivyo ni lazima nchi iwe na
kanuni na taratibu zitakazotumika kuhakikisha vipimo sahihi kwa maslahi ya
wadau wote wa sekta hiyo, ikiwa ni pamoja na serikali, kupitia Mamlaka ya
Mapato (TRA) kuweza kukusanya mapato halisi kwa kutumia vipimo sahihi.
Katika hotuba yake ya mwisho wa mwezi Agosti mwaka jana Dkt. Kikwete anasema Serikali imejipanga kukabiliana na changamoto zinazoambatana na ugunduzi wa gesi asilia nchini. Rais anasema hadi sasa, Tanzania imeshagundua kati ya futi za ujazo trilioni 25.4 na trilioni 28.9 ambazo zikitumika vizuri, zinaweza kubadili uchumi na maisha ya Watanzania. Chuwa anasema kwamba kanuni hiyo ya matumizi ya gesi imekuja kufuatia mapungufu makubwa katika usimamizi wa vipimo mbalimbali hapa nchini katika sekta ya gesi asilia hapa nchini.
Kwa upande wa gesi ya matumizi ya
majumbani (LPG) anasema kwamba wamekuwa
wakikabiliana na mapungufu mbalimbali ili kuhakikisha kwamba gesi anayouziwa
mteja ina vipimo sahihi.
Anasema taasisi yake imekuwa ikitoa
elimu kwa wadau juu ya umuhimu wa kuzingatia vipimo sanjari na kuchukua hatua
mbalimbali kwa mujibu wa kanuni ili kukabiliana na tatizo hilo ikiwamo kufanya
ukaguzi wa ujazo wa gesi kwenye mitungi kwa wasambazaji mbalimbali.
“Inatakiwa mteja akitaka kuhakiki
uzito wa mtungi apate taarifa zote muhimu zinazohusu gesi yenyewe (net weight)
na ipi inayohusu uzito wa gesi pamoja na mtungi wake (gross weight) au uzito wa
mtungi peke yake (tare weight),”anafafanua hivyo na kuongeza kuwa sasa kanuni
imeweka utaratibu unaotambulika kwa wadau wote”.
Anasisitiza kwamba makampuni yote yanayosambaza gesi ya kupikia majumbani yanapaswa kuweka kwenye chapa yao uzito wa mtungi wakati hauna gesi, uzito wa gesi peke yake na uzito wa jumla yaani wa mtungi na gesi...Tutaendelea kesho. |
March 30, 2015
KUTOKA WAKALA WA VIPIMO (WMA):SERIKALI KUPITIA WAKALA WA VIPIMO YAHAKIKISHA WANANCHI WANAPATA HUDUMA BORA ZA VIPIMO
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment