Ofisa Mkuu wa Uendeshaji wa Kampuni ya Uwekezaji ya UTT-AMIS, Migangala Simon.
UTT-AMIS NI NINI?
UTT-AMIS ni taasisi ya
serikali iliyo chini ya Wizara ya Fedha, dhumumi kuu la kuanzishwa kwake ni
kuanzisha na kuendesha Mifuko ya Uwekezaji wa Pamoja hapa nchini ili
kuwawezesha wananchi kiuchumi kutokana
na uwekezaji wa pamoja.
Mtanzania aliye ndani au nje ya nchi ikijumuisha mtu binafsi (wakiwamo watoto)
wawekezaji wasiokuwa watu binafsi (taasisi au makampuni) kama vile taasisi za
mifuko ya jamii,benki,taasisi za kiserikali, vyombo vya ulinzi na
usalama,mashirika yasiyokuwa ya kiserikali asasi za kiraia au mashirika mengine ni miongoni mwa walengwa wa
taasisi hiyo.
Mbali ya Makao Makuu ya UTT-AMIS kuwa Jijini Dar es
Salaam, Jengo la Sukari maarufu kama Sukari
House, pia wana ofisi katika Mikoa ya Mwanza, Arusha, Dodoma , Mbeya na
Zanzibar na kwamba Ofisi zote za mikoani zipo
katika majengo ya Shirika la Posta ya Mikoa hiyo.
No comments:
Post a Comment