Utafiti mpya umebaini kuwa wakazi wa Mkoa wa Kilimanjaro
wanaongoza kwa unywaji wa pombe hasa ya viroba, ikiwa ni mara nne
zaidi ya wakazi wanaokunywa pombe katika mikoa ya Mwanza na Geita.
Katika utafiti huo uliofanywa na Taasisi ya Taifa
ya Utafiri wa Magonjwa ya Binadamu (NIMR) kupitia mradi wa Strive
ulibaini kuwa idadi kubwa ya wanaokunywa pombe ni vijana wenye umri wa
kati ya miaka 15 hadi 24.
Utafiti huo wa NIMR ulilenga kujua ukubwa wa
Matumizi ya Pombe kwa vijana katika mikoa ya Kilimanjaro, Mwanza,
Geita na Kahama umebaini kuwa mkoa wa Kilimanjaro unaongoza kwa unywaji
wa pombe kwa vijana wenye umri kutokana na utamaduni uliopo mkoa huo.
Akitoa matokeo ya utafiti huo uliopewa jina la
ripoti ya utafiti wa ukubwa wa matumizi ya pombe nchi, Dar es Salaam,
Mtafiti wa NIMR Dk Saidi Kapiga alisema hapa nchini matumizi ya pombe
ni makubwa na wanaume wanaongoza kwa kunywaji wa pombe kuliko wanawake
licha ya kuwa na madhara kwa watumiaji.
“Hapa nchini matumizi ya kiwango cha pombe ni
makubwa na wanaume wanaongoza kwa utumiaji wa pombe kwa asilimia 25 hadi
30 ikilinganishwa na wanawake ambao ni asilimia 8 hadi 15 na hii ni kwa
mujibu wa utafiti uliofanywa na wizara ya afya na ustawi wa jamii miaka
miwili iliyopita”alisema Dk Kapiga.
No comments:
Post a Comment