Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Jakaya Kikwete akizungumza
na Afisa Mtendaji mkuu wa Wakala wa Vipimo Bi. Magdalena Chuwa
alipotembelea banda la Wizara ya Viwanda na Biashara kwenye kilele cha
maadhimisho ya siku ya Wanawake Duniani hivi karibuni
Leo katika Makala yetu haya kutoka Wakala wa Vipimo (WMA),Afisa Mtendaji Mkuu wa WMA Bi.Magdalena Chuwa anazungumzia Mizani
kwenye huduma mbalimbali,fuatana naye hapa chini.....
Anasema Wakala pia una mikakati endelevu ya kuhakikisha
kwamba vipimo katika mizani ni sahihi na mara kwa mara maofisa wa Wakala wamekuwa wakifanya ukaguzi wa mizani
ili kuhakikisha ina toa vipimo sahihi kwa mujibu wa sheria.
Anazitaja mbinu mbalimbali ambazo baadhi ya wauzaji
wa wanaotumia mizani wamekuwa wakizitumia kwa
lengo la kuwaibia wananchi.
Mbinu hizo ni pamoja na kutumia mawe yenye uzito
pungufu,kutumia mizani yenye muundo usiokubalika kisheria,kutumia mizani au
mawe yasiyokuwa na muhuri wa Serikali.
Nyingine ni kuchezea mizani kama vile, kutegua pini,
kunatisha nyama kwenye sahani,kuweka sumaku,kufunga uzi kwenye beam ya mizani
upande wa sahani,kutumia kisu kuinua mizani upande wa mawe, kufungulia feni
upande wa sahani,kutumia na vitu visivyoruhusiwa badala ya mawe kama vile
majani ya chai n.k.
|
March 26, 2015
KUTOKA WAKALA WA VIPIMO (WMA):SERIKALI KUPITIA WAKALA WA VIPIMO YAHAKIKISHA WANANCHI WANAPATA HUDUMA BORA ZA VIPIMO
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment