KWA MAONI AU USHAURI E-mail: inocomm2014@gmail.com, PIGA SIMU: 0714555668

www.utt-pid.org


TEMBELEA: www.utt-pid.org

March 28, 2015

LOWASSA AWAKOROGA MASHEIKH BAGAMOYO


NA MWANDISHI WETU
SIKU chache baada ya Baraza Kuu la Waislam Tanzania (BAKWATA) Wilaya ya Bagamoyo kuwakana masheikh 50 kutoka wilayani humo waliokwenda mjini Dodoma kumshawishi Waziri Mkuu wa zamani, Edward Lowassa kugombea urais, masheikh hao wamejitokeza na kuthibitisha kutambuliwa kwao na BAKWATA.
Msemaji Mkuu wa masheikh hao, Alhaji Hassan Kilemba jana aliitisha mkutano wa waandishi wa habari mjini Bagamoyo akielezea kusikitishwa na kauli iliyotolewa na Sheikh Mkuu wa Bagamoyo, Abdulkadir Ramiya ikikana kuwatambua.
Alisema kauli ya Sheikh Ramiya imewasikitisha kwa sababu imewavunjia heshima na kuwafanya waonekana watu wasiofaa mbele ya jamii kwa kutambulika kuwa ni Masheikh wa bandia wakati wanatambuliwa na BAKWATA.
“Sisi pamoja na kuungama wazi kuwa safari yetu haikuwa na msukumo wowote wa BAKWATA Wilaya ya Bagamoyo, ajabu Sheikh Mkuu wa Wilaya ya Bagamoyo ambaye pia ni Sheikh wa Tarikatul Kadirya aliitambua safari yetu kwa sababu tulimpa taarifa kabla ya kuianza.
“Tumesikitishwa na kauli ya Sheikh Mkuu kuwa haitambua safari yetu ya Dodoma wakati tulimtaarifu kabla na akatukubalia…ametugeuka baada ya vigogo wa CCM kumfuata,” alisema Sheikh Kilemba.ZAIDI MTANZANIA

No comments:

Post a Comment