Mchungaji Josephat Gwajima.
MCHUNGAJI Kiongozi wa Kanisa la Uzima na Ufufuo, Josephat Gwajima leo
amejisalimisha kituo cha polisi kati kuhojiwa juu ya kutoa lugha chafu
dhidi ya Askofu Mkuu wa Kanisa Katoliki Jimbo Kuu la Dar es Salaam,
Muadhama Polycarp Kardinali Pengo.
Gwajima alirekodiwa kwenye ibada ya kanisa lake Jumapili iliyopita
ambapo ‘alimtusi’ Pengo akituhumu kuwa ni msaliti kwani amekwenda
kinyume na Taasisi ya Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania (TEC), Baraza
la Makanisa ya Kipentekoste (CPCT) na Jumuiya ya Kikristo Tanzania
(CCT) kwa kuwataka waumini waisome Katiba Inayopendekezwa kisha wapewe
uhuru wa kupiga kura ya “ndiyo” au “hapana” tofauti na vyombo hivyo
vyenye dhamana ya kuongoza dini ya Kikristo vilivyotaka waumini waipigie
kura ya “hapana” Katiba Inayopendekezwa.
|
March 27, 2015
MCHUNGAJI GWAJIMA AJISALIMISHA POLISI
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment