Shirikisho
la Mpira wa Miguu nchini TFF, limetangza viingilio vya mchezo wa siku
ya jumapili kati ya Taifa Stars (Tanzania) dhidi ya The Flames (Malawi)
utakaochezwa kwenye uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza kuwa ni tsh.
5,000 mzunguko na tsh. 12,000 kwa jukwa kuu.
Kuelekea mchezo huo wa jumapili
kikosi cha timu ya Taifa ya Tanzania (Taifa Stars) inayodhaminiwa na Bia
ya Kilimanjaro, kimeendelea na mazoezi katika Uwanja wa CCM Kirumba
huku wachezaji wake wote wakiwa na ari na morali ya juu tayari kwa
kuwakabili the Flames.
Taifa Stars iliyo chini ya kocha
mkuu Mart Nooij iliwasili jijini Mwanza siku ya jumanne na kufikia
katika hoteli ya La Kairo iliyopo eneo la Kirumba,
ikiwa na kikosi kamili kwa ajili ya mchezo huo wa kirafiki wa Kimataifa uliopo kwenye kalenda ya FIFA.
Maandalizi ya mchezo kwa upande wa
Taifa Stars yamekamilika, timu imekua ikifanya mazoezi katika uwanja wa
CCM Kirumba ambao ndio uwanja utakaotumika kwa mchezo.
Wachezaji waliopo jijini Mwanza ni
, Aishi Manula, Mwadini Ali, Shomari Kapombe, Erasto Nyoni, Aggrey
Morris, Oscar Joshua, Nadir Haroub, Salim Mbonde, Haji Makame, Hassan
Isihaka na Abdi Banda.
Wengine ni Mwinyi Kazimoto, Haroun
Chanongo, Mrisho Ngasa, Salum Abubakar, Amri Kiemba, Frank Domayo, Said
Ndemla, John Bocco, Juma Luizio, Thomas Ulimwengu na Mbwana Samatta.
MALAWI YAWASILI MWANZA
Timu ya Taifa ya Malawi (The
Flames) tayari imewasili leo jijini Mwanza majira ya saa sita mchana,
ikiwa na kikosi chake kamili kwa ajili ya mchezo dhidi ya Taifa Stars
siku ya jumapili kwenye Uwanja wa CCM Kirumba.
Malawi imewasili ikiwa na kikosi
chake kamili cha wachezaji 18 na kufikia katika hotel ya JB Belimonte,
wakiwemo wachezaji saba wanaocheza soka la kulipwa katika nchi za Afrika
Kusini, Congo DR, Msumbuji na Zimbabwe.
Wachezaji wa kimataifa waliowasili
ni nahodha Joseph Kamwendo (TP Mazembe -Congo DR), Chimango Kayira
(Costal de Soul – Msumbiji), Frank Banda (HBC Songo – Msumbiji), Esau
Kanyenda (Polokwane City – Afrika Kusini), Harry Nyirenda (Black
Leopards – Afrika Kusini), Limbikani Mzava (Celtic – Afrika Kusini)
Gerald Phiri (Caps United – Zimbambwe)
Wegine ni McDonald Harawa (Hoyale
FC), Richard Chipuwa (Wanderers), Lucky Malata (Silver), John Lanjesi
(Civo), Francis Mulimbika (Wanderers), John Banda (Blue Eagle), Earnest
Tambwe (Surestream) , Micium Mhone (Blue Eagle), Chikoti Chiriwa (Red
Lions), Peter Wadabwa (Silver) na Amos Khamula(Support Ballaton)
Mkuu wa msafara ni Alexander Waya,
Kocha mkuu Young Chimodzi, kocha msaidizi Jack Chamangwana, kocha wa
makipa Pillip Nyasulu, Daktari wa timu Levison Mwale, Meneja wa timu
Frank Ndawa na Afisa Habari James Sangala.
Kikosi cha timu ya Taifa ya Malawi
kinatarajiwa kufanya mazoezi leo saa 10 jioni katika uwanja wa CCM
Kirumba, huku siku ya jumamosi wakipata nafasi ya kufanya mazoezi tena
kwenye uwanja huo wa mchezo.
Kesho jumamosi saa 5 kamili
asubuhi kutafanyika mkutano na waandishi wa habari katika hoteli ya La
Kairo iliyopo Kirumba jijini Mwanza, kocha wa Stars Mart Nooij na kocha
wa The Flames Young Chimodzi wataongelea maandilizi ya mchezo wao wa
siku ya jumapili.
No comments:
Post a Comment