Na Mwandishi Wetu, Afrika Kusini. MWENYEKITI mpya wa Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC), Amina Mwidau, ameongoza wajumbe wa kamati hiyo kwa kufanya ziara nchini ya Afrika Kusini. Wakiwa nchini humo walitembelea Bandari ya Durban, ambapo walifanya mazungumzo na viongozi wa juu wa bandari hiyo wakiongozwa na Meneja wake Vusi Khumalo. Mwidau ambaye ameambatana na wajumbe kadhaa wa PAC akiwemo Makamu Mwenyekiti Deo Filikunjombe, Mbunge wa Tabora Mjini, Ismail Aden Rage pamoja na Mbunge wa Mbinga Mashariki, Gaudence Kayombo. |
Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC), Amina Mwidau akiwa na Meneja wa Bandari Durban nchini Afrika Kusini, Vusi Khumalo wakati kamati hiyo ilipofanya ziara ya kikazi nchini humo, Machi 24 na 25 mwaka huu |
Mwidau akiwa na wajumbe wa PAC, Ismail Rage pamoja na Gaudence Kayombo wakipata maelezo. |
No comments:
Post a Comment