Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam
MKUU wa Wilaya ya Kinondoni, Paul Makonda amemwandikia barua Askofu
wa Kanisa la Ufufuo na Uzima, Josephat Gwajima akimtaka afike mbele ya
Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Wilaya kwa mahojiano. Inaelezwa kuwa
Makonda alimtumia Askofu Gwajima barua hiyo Machi 30 mwaka huu, akiwa
amelazwa katika Hospitali ya TMJ. Hata hivyo, kiongozi huyo wa kiroho
amegoma akisema hawezikwenda ofisini kwa mkuu huyo wa wilaya kwa
mahojiano. Mmoja wa wasaidizi wa Askofu Gwajima aliliambia MTANZANIA
jana kuwa hatua ya Makonda kumtumia barua haikumpendeza kiongozi huyo wa
kanisa. “Makonda alikuja katika Hospitali ya TMJ na kudai amekuja
kumwona Askofu Gwajima huku akiwa amebeba barua yake. Baada ya kumwuliza
hali ya maendeleo ya afya yake alitoa barua na kumkabidhi jambo ambalo
halikuwa jema. “Baada ya muda Askofu Gwajima alituita wasaidizi wake na
kutueleza kuwa amepewa barua ya wito kwa DC, sasa tukajiuliza askofu
anaumwa. Je, inakuaje aende tena katika mahojiano na mkuu wa wilaya? “Na
kama ni hivyo nini kazi ya polisi maana wamemuhoji tangu siku ya kwanza
baada ya kumkamata. Je, inakuaje tena Makonda alete barua ya kumtaka
askofu akahojiwe tena mbele ya Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Wilaya
mbele ya DC? “Hapa kuna mchezo unataka kufanywa na je, katika masuala
haya ya usalama sijui kama huyo DC anajua wajibu wake. Mtu anahojiwa na
polisi sasa inakuaje tena aitwe na DC ahojiwe na kamati ya ulinzi?
Amesema hatokwenda,”CHANZO:MTANZANIA
No comments:
Post a Comment