Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Jakaya Kikwete akizungumza
na Afisa Mtendaji mkuu wa Wakala wa Vipimo Bi. Magdalena Chuwa
alipotembelea banda la Wizara ya Viwanda na Biashara kwenye kilele cha
maadhimisho ya siku ya Wanawake Duniani hivi karibuni Sehemu iliyopita ya makala haya tulizungumzia mbinu wanazozitumia baadhi ya wauzaji wasio waaminifu wanaochezea mizani ili kujipatia faida kubwa, leo katika sehemu hii ya mwisho Afisa Mtendaji Mkuu wa WMA Bi.Magdalena Chuwa anatueleza suluhisho la tatizo hilo. Fuatana naye....
Suluhisho
Chuwa anasema
kutokana na udanganyifu huo uliokithiri kwenye mabucha, Wakala wa
Vipimo umekuwa ukitoa mapendekezo mbalimbali ikiwa ni pamoja na yafuatayo.
Wamiliki wa bucha kuajiri rasmi wauzaji wa nyama
katika bucha kwa mujibu wa sheria ya kazi. pia wamiliki na wauzaji wa mabucha
kukaa pamoja kujadiliana namna ya kuboresha huduma zao na chama cha wamiliki wa
mabucha kuhakikisha mapendekezo hayo yanatekelezwa.
Mapendekezo mengine ni Wizara ya Kazi na Ajira
ifanye ukaguzi wa mara kwa mara kwenye mabucha kuhakikisha kwamba kuwa wauzaji
wa nyama kayika bucha hizo wanazo ajira rasmi na haki za msingi na mahusiano
zinafuatwa.
Mwisho
|
April 2, 2015
KUTOKA WAKALA WA VIPIMO (WMA):SERIKALI KUPITIA WAKALA WA VIPIMO YAHAKIKISHA WANANCHI WANAPATA HUDUMA
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment