Muhammadu Buhari, rais mteule wa Nigeria |
Rais mteule wa Nigeria, Muhammadu
Buhari, amezitaja vurugu zinazosababishwa na kundi la wanamgambo wa
Kiislamu wa Boko Haram kuwa ni tatizo kubwa linalokabili nchi.
Katika
mahojiano maalumu na BBC, kiongozi huyo mstaafu wa jeshi amesema
anatarajia kulishinda kundi hilo baada ya dhamira mpya kutoka jeshini na
msaada wa nchi jirani. "Kwa ushirikiano na majirani zetu Cameroon,
Chad, Niger na jumuia ya kimataifa na dhamira ambayo tutapata kutoka
katika jeshi, Nafikiri itachukua muda mfupi zaidi kukabiliana nao."
Jenerali
Buhari amesema tayari ameainisha msingi wa tatizo linalokabili nchi ya
Nigeria, lakini amewataka raia wa nchi hiyo kuwa wavumilivu.
"Tumebaini
matatizo makubwa matatu. Ambayo ni kukosekana kwa usalama nchini,
tatizo ambalo kila mmoja analifahamu na lingine ni ukosefu wa ajira, hii
ina maana uharibifu wa uchumi ikiwa ni kutokana na vitendo vya rushwa
na rushwa yenyewe. Matatizo haya matatu makuu, Wanigeria wote wanafahamu
na tunaomba ushirikiano wa wananchi wa Nigeria, wasitarajie miujiza
kutokea katika kuyapatia ufumbuzi matatizo haya katika kipindi cha miezi
michache baada ya kutwaa madaraka kwa sababu uharibifu umechukua miaka
mingi, miaka kumi na sita ya utawala wa chama tawala cha nchi hii."
Anasema rais huyo mteule wa Nigeria.BBC
No comments:
Post a Comment