SHIRIKISHO LA NGUMI TANZANIA
Yah:-
Timu ya Taifa ya Ngumi 2015.
Hatimaye
baada ya mchakato wa muda mrefu,
uliofanyika kwa umakini kwa kuzingatia vigezo vilivyowekwa hatimaye
Shirikisho la Ngumi Tanzania (BFT) limepata wachezaji wa timu ya Taifa ya Ngumi
2015. Katika mashindano ya kimataifa
yaliyoshirikisha timu za taifa kutoka Uganda na Kenya, mashindano yaliyomalizika
kwa mafanikio, Jumamosi ya tarehe 28.03.2015 uwanja wa Taifa wa ndani .
Mabondia
waliochaguliwa kwa sasa taratibu za kuombewa ruhusa katika timu zao zinafanyika
na taratibu hizo zitakapo kamilika watatakiwa kuanza mazoezi kabla ya tarehe
15.04.2015, kwa ajili ya kushiliki mashindano mbalimbali ya kitaifa na
kimataifa hasa mashindano ya Michezo ya
Afrika (All African Games) Septemba 4-19. Brazzaville Congo. Na mashindano ya
Ubingwa wa Dunia (AIBA World Boxing Championships) Octoba 5-18 Doha Qatar.
Nakala kwenu
kwa Taarifa.
Makore
Mashaga
Katibu Mkuu
(BFT)
No comments:
Post a Comment