Walisema iwapo ataidhinishwa na vikao vya juu vya chama kupambana na wagombea wengine wa vyama vya upinzani, hawatampa ushirikiano badala yake watamuunga mkono mgombea wao wa nafasi ya urais pekee.
Akizungumza kwa niaba ya wenzake, mmoja wa wagombea hao, Chifu Msopa, alisema ushindi aliopata Saru katika kura za maoni haukuwa halali ndiyo maana hadi sasa wamegoma kuweka saini ya kukubali matokeo.
Alisema wanaviomba vikao vya juu vya CCM kutoa tamko juu ya matatizo yaliyojitokeza wilayani Handeni kwani uchaguzi huo ulitawaliwa na vitendo vya rushwa ambavyo vilinyamaziwa na uongozi husika.
“Mgombea wetu wa urais, John Magufuli atapata kura za kishindo, lakini ubunge hatutampa Saru endapo chama kitampitisha kwani ushindi wake si halali na umejaa ukiukwaji mkubwa, hivyo tunakiomba chama kifanye uchunguzi na kiwapitishe wagombea wanaokubalika hapa jimboni,” alisema Msopa.
Katibu wa CCM wilayani humo, Saleh Kikwehu, alipoulizwa kuhusu tuhuma hizo, alisema wanaendelea na vikao kusikiliza malalamiko hayo huku akisema yeye si msemaji wa suala hilo kwakuwa hivi sasa lipo katika ngazi
ya mkoa.
Mtanzania.
No comments:
Post a Comment