Mwenyekiti wa CCM Taifa Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akiongoza kikao cha Kamati kuu ya CCM kilchofanyika katika ukumbi wa White house, Makao Makuu ya CCM mjini Dodoma jana. |
CHAMA
Cha Mapinduzi (CCM) kimeagiza kurudiwa kwa kura za maoni kesho katika
majimbo matano nchini, kutokana na dosari mbalimbali zilizojitokeza
wakati wa mchakato wa upigaji kura hizo.
Wakati
agizo hilo likitolewa kwa majimbo husika, hatma ya watakaopeperusha
bendera ya CCM katika ubunge, udiwani na Wawakilishi inatarajiwa
kujulikana wakati wowote kuanzia sasa baada ya vikao vya chama kuanza
vikao vyake mjini Dodoma jana.
Kamati
Kuu ya chama hicho, ambacho kimesema kipo vizuri na kwamba vikao vyake
vya kupata wagombea vinakwenda vizuri, ilitoa jana maagizo ya kurudiwa
uchaguzi huo baada ya Mwenyekiti, Rais Jakaya Kikwete kufungua kikao
hicho.
Katibu wa
Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye aliwaambia waandishi wa habari kwamba
majimbo yaliyokumbwa na dosari hizo na ambayo yanatakiwa kurudia
uchaguzi kesho ni Rufiji mkoa wa Pwani, Kilolo mkoa wa Iringa, Makete
mkoa wa Njombe, Busega mkoa wa Simiyu na Ukonga mkoa wa Dar es Salaam.
Akitoa
maelekezo hayo ya chama, alisema kikao cha Kamati ya Maadili
kilimalizika juzi usiku na kwamba jana kikao cha Kamati Kuu kilianza.
Alisema kama kitakuwa kimefanikiwa kumaliza, leo kitaanza kikao cha
Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC).
“Majimbo
matano yanatakiwa kurudia kura za maoni Alhamisi Agosti 13 baada ya
kutokea dosari mbalimbali...baada ya marudio ya kura hizo yanatakiwa
kuleta matokeo kwa ajili ya uamuzi,” alisema.
No comments:
Post a Comment