Aliyekuwa mshindi wa kura za maoni Bunda Mjini wa Chadema, Pius Masururi ametangaza kukihama chama hicho na kujiunga CCM huku mwenyekiti wa jimbo hilo, Samuel Imanani na wanachama 50 wakiwamo viongozi wakijivua uanachama.
Masururi,
aliyepata kura 65 mbele ya wapinzani wake wa karibu, Magembe Makoye
(40) na Ester Bulaya (37) katika kura za maoni zilizopigwa Julai 29
mwaka huu, ametangaza uamuzi wake huo jana kupitia kituo cha redio cha
Mazingira FM cha mjini Bunda.
Masururi
amesema ameamua kukihama chama hicho baada ya kutofurahiswa na kitendo
cha Kamati Kuu ya Chadema kupuuza uamuzi wa wanachama kwa kukata jina la
aliyeshinda kura za maoni.
Katika
jimbo la Bunda Mjini, Chadema imebadilisha matokeo na kumteua mshindi
wa tatu, Ester Bulaya kupeperusha bendera ya chama hicho, jambo
lililowaudhi baadhi ya makada wake.
Baadhi
ya wanachama walioongozwa na mwenyekiti wa jimbo hilo, Samuel Imanani
wamesema kitendo cha makao makuu ya Chadema kutengua uamuzi wa kura zao
za maoni ni udhalilishaji mkubwa, hivyo hawana budi kukihama chama
hicho.
“Tumeamua
kuuachia uongozi wa makao makuu uendeshe mambo yote, nasi tusiwe tena
wanachama maana hautusikilizwi,” alisema Mashaka Kipili mmoja wa
wanachama hao.
No comments:
Post a Comment