………………………………………………………………………………………
Shirikisho la Ngumi
za kulipwa la Afrika (IBF Africa) kwa kushirikiana na Ta
asisi ya Miss
Tanzania 2012, Brigitte Alfred Foundation (BAF) na kampuni ya Kango
wameandaa mapambano ya ngumi ya kimataifa kwa kushirikisha mabondia
nyota duniani.
Mapmbano hayo yamepangwa
kufanyika Novemba 28 kwenye ukumbi wa Mlimani City na lengo lake kubwa
ni kutafuta fedha za kusaidia watu wenye ulemavu wa ngozi (albino).
Rais wa IBF Africa, Onesmo
Ngowi alisema kuwa siku hiyo imepewa jina la “knock out albinos
killers” (piga wanaua albino) ambapo bondia kutoka Denmark, Lolenga Mock
atapigana na bondia nyota wa Zambia, Chioctha Chimwemwe katika pambano
la uzito wa super middle la IBF continental Africa super.
Pambano hilo limepangwa kuwa la
raundi 12 na litafuatiwa na pambano lingine la kulipiza kisasi kati ya
bondia kutoka Afrika Kusini, Phillip Ndou atakayepambana na Mtanzania,
Ramadhan Shauri kuwania ubingwa wa IBF-Continental Africa welterweight
ambalo pia litakuwa la raundi 12.
Bondia nyota wa Tanzania,
Cosmas Cheka naye atapanda ulingoni kupambana na Gottlieb Ndokosho wa
Namibia kuwania ubingwa wa IBF continental Africa super-feather.
Mabondia wa Kenya, Geoffrey
Munika na James Onyango nao wataingia ulingoni kupambana na mabondia
kutoka china na Iran ambao watajulikana baadaye.
Pia kutakuwa na pambano mengine
ambayo yatawakutanisha mabondia wanawake, Lulu Kayage dhidi ya bondia
atakayetangazwa baadaye kuwania ubingwa wa IBF Africa flyweight.
“Lengo ni kutafuta fedha za
kuchangia kununua vifaa maalum kwa albino na mpaka sasa maandalizi
yanaenda vizuri, hii ni tukio kubwa sana kwa ngumi za kulipwa hapa
nchini,” alisema Ngowi.
Alisema kuwa wameamua
kushirikiana na Brigitte kutokana na kutambua juhudi zake za kutetea
albino baada ya kuwajengea bweni eneo la Buhangija, Shinyanga na taasisi
yake kwa kushirikiana na Junior Achievements (JA) wanatoa elimu ya
ujasiriamali kwa jamii hiyo.
“Brigitte akiwa mwenye
mashindano ya urembo ya dunia, 2012, aliweka rekodi ya kushika nafasi ya
tatu katika mashindano ya ‘urembo wenye malengo maalum” au Beuty with
purpose”, alipeleka kazi yake ya ujenzi wa bweni la albino mkoani
shinyanga, imetupa faraja sana na kuamua kumuunga mkono katika vita
hiyo,” alisema.
Brigitte alishukuru kuungwa
mkono na kuomba wadhamini kujitokeza kusaidia shughuli hiyo ambayo baada
ya ngumi, pia kutakuwa na mbio za marathon mkoani Kilimanjaro zenye
lengo hilo hilo.
“Tumeandaa mbio za Marathon
mkoani Kilimanjaro wiki moja baada ya ngumi, mbali yam bio hizo, pia
kutakuwa na zoezi la kupanda mlima Kilimanjaro, lengo ni kutafuta fedha
na vile vile kutangaza utalii wetu, naomba makampuni yajitokeze,”
alisema Brigitte.
No comments:
Post a Comment