Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Msaada wa Sheria kwa Wanawake na Watoto (WLAC), Theodosia Muhulo Nshala, akizungumza na wanahabari katika kongamano hilo. |
Mmoja wa washiriki wa kongamano hilo, Kuruthum Dindili (katikati), akizungumza na wanahabari katika kongamano hilo. |
Kongamano likiendelea. |
……………………………………………………………………………
Na Dotto Mwaibale
WALEMAVU
wenye mahitaji maalum wameonekana kusahaulika na serikali kwa
kuwawezesha kufikia haki zao kama mchakato wa kupiga kura kutokana na
kukosekana kwa miundombinu rafiki.
Kauli
hiyo imetolewa Dar es Salaam leo asubuhi na Mkurugenzi Mtendaji wa
Kituo cha Msaada wa Sheria kwa Wanawake na Watoto (WLAC), Theodosia
Muhulo wakati wa mafunzo kwa wanawake walemavu wenye mahitaji maalum
kuelekea uchaguzi.
Lengo
ikiwa ni ushiriki wa wanawake wenye mahitaji maalum katika kushiriki na
kujitokeza katika mchakato wa uchaguzi mkuu unaotarajia kufanyika
Oktoba 25,mwaka huu pamoja na kujenga na kukuza uelewa.
“Kundi
hili limesahaulika kwa serikali yetu hivyo kwa kuwapa semina hii
kunawafanya wasionekane kutengwa na jamii ndiyo maana tumeona tuwaite na
kuwaongezea uelewa wao katika kushiriki uchaguzi mkuu ikiwa ni pamoja
na kushiriki,kuchagua na kuchaguliwa,”alisema
Alisema
serikali inapaswa kujua mahitaji ya walemavu kwenye michakato ya
jamii,kwani hakuna sehemu maalum ya watu wa kundi hilo kwa kuwawekea
miundombinu kama sehemu zenye ngazi ili kuweza kufika bila tatizo
lolote.
Muhulo
alisema wanawake wanapaswa wajitokeze kupiga kura ili waweze kuchagua
na kuchaguliwa kwa kumshagua rais, wabunge na diwani ili waweze
kuletewa maendeleo na mabadiliko katika jamii zao na si kubaki nyuma.
Kwa
upande wake Mbunge wa viti Maalum kupitia Umoja wa Wazazi nchini wa
Chama cha Mapinduzi,Kuruthumu Dindili, alimpongeza rais Kikwete
anayemaliza muda wake kwa kuwa ni mpenzi wa watu lakini walikosa wa
kuwawakilisha bungeni kwani anaamini wangefaidika.
“Kwa
bunge lilikopita hatukuwa na mwakilishi bungeni wa kuweza kutusemea
malalamiko yetu hasa kwa watu wenye ulemavu wa viungo kwa maana
wangekuwepo tungefaidika na mambo mengi sana, walikuwa wamekaa tu kimya
bungeni wenzetu wananufaika wao…sisi walemavu hakuna tuanachokipata
kupitia wao ndio maana tumeona tuingie na sisi kwenye mchakato,”alisema
Alisema
wanapojitoa kugombea nafasi mbalimbali za kiuongozi wanaonekana ni
kichekesho kwa wale wasiokuwa walemavu na kuwabeza kwa kukosa fedha za
kufanyia kampeni, aliitaka serikali kwa kutoa nafasi nyingi za
wawakilishi walemavu katika bunge lijalo ili kuwe na sauti nyingi za
kuleta maendekeo ya kupata mahitaji ya kimsingi kuanzia ngazi za afya,
elimu.
Aidha
semina hiyo ilihudhuliwa na Chama cha walemavu wa viungo(Chawata),
Chama cha Walemavu wa Ngozi(Tas), Chama cha Wasioona (TLD), Chama cha
Viziwi Wasioona(Tasodep), Chama cha wazazi wenye watoto wenye vichwa
vikubwa na mgongo wazi(Asbat) pamoja na Chama cha Afya na Akili(Tuspo).
No comments:
Post a Comment