…………………………………………………………………………
Na Jenikisa Ndile-MAELEZO
Watanzania wameaswa kuzingatia
namna bora ya kuhifadhi mazingira, upangaji wa matumizi bora ya ardhi na
utekelezaji wa mipango ili kuleta tija na maendeleo endelevu nchini.
Kauli hiyo imetolewa na Katibu
Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais Bw. Sazi Salula leo jijini Dar es salaam
alipokuwa akifungua Mkutano wa wadau wa mazingira unaohusu utekelezaji
wa miradi ya majaribio ya Mkakati wa Kupunguza Uharibifu wa Misitu
(MKUHUMI) nchini.
Bw. Sazi alisema kuwa mipango
hiyo ya MKUHUMI inalengo la kuondoa umasikini kwa watanzania waishio
vijijini ambao wapo karibu na hifadhi za misitu inasimamiwa na
kutekelezwa kwa kushirikiana na Serikari ya kijiji ili kuhakikisha
mafanikio yanapatikana kwa kuzingatia utekelezaji na usimamizi wa sheria
kupitia kamati za vijiji.
Majaribio ya sera ya mazingira
yamefadhiliwa na Serikali ya Tanzania kwa kushirikiana na Serikali ya
Norway ili kuboresha na kushughulikia masuwala ya ardhi, misitu na
kupunguza gesi joto kwa kuhimiza jamii kupanda miti kwa shughuli za
maendeleo endelevu nchini.
Mipango hiyo inatekelezwa katika
wilaya za Sumbawanga, Lindi, Kilwa, Zanzibar, Pemba, Kigoma na Kondoa
ambapo sera hiyo imewapa elimu ya kujenga utayari wa shughuli za MKUHUMA
na kuwezesha ushiriki mpana wa wadau ili kufikia malengo
yaliyokusudiwa.
Kwa upande wake Kiongozi wa
miradi ya majaribio ya MKUHUMI Merja Makela alisema kuwa taasisi yake
imefanikiwa kutokana na kusimamia miradi hiyo ambayo imepokelewa na
kutekelezwa kama ilivyopangwa katika maeneo husika nchini.
Naye Mkurugenzi wa Mazingira
kutoka Ofisi ya Makamu wa Rais Dkt. Julius Ningu alisema kuwa kwa
tathmini iliyofanyika mwaka 2013, asilimia 55 ya ardhi ya Tanzania
imefunukwa na misitu ambapo juhudi zinaendelea kufanyika kwa
kuwaelimisha watanzania kuendelea kuitunza misitu hiyo kwa manufaa ya
sasa na baadaye.
No comments:
Post a Comment