Na Mwandishi wetu-MAELEZO
Katibu Mkuu Kiongozi
Balozi Ombeni Sefue anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika ufunguzi wa
michezo ya Wizara, Idara zinazojitegemea ,Wakala wa Serikali na Ofisi
za wakuu wa Mikoa (SHIMIWI) itakayoanza Jumamosi ijayo(15.8.2015) mjini
Morogoro.
Kwa mujibu wa taarifa
kwa vyombo vya habari iliyotolewa leo jijini Dar es salaam na Kaimu
Katibu Mkuu SHIMIWI Moshi Makuka, mashindano ya mwaka huu yatafanyika
kwa wiki mbili.
Amesema kuwa siku ya
ufunguzi kutakuwa na michezo ya mpira wa miguu kati ya Elimu na Hazina
kwa wanaume , mpira wa pete utazikutanisha timu ya Afya na Mambo ya
Ndani.
Makuka ameongeza kuwa
siku hiyo pia kutakuwepo mchezo wa kuvuta kamba kati ya Wakala wa
Jiolojia Tanzania na Mambo ya Nje kwa wanaume na kamba kwa wananwake
kati ya Ikulu na Bunge.
Amezitaja timu
zilizothibitisha kushiriki kuwa ni Ikulu, Utumishi, Waziri Mkuu, Afya,
Ardhi, Elimu, Hazina, Kilimo,TAMISEMI, Mifugo, Maji, Afika mashariki,
Maliasili, Mambo ya Nje, Mambo ya Ndani, Ulinzi, Nishati, Maendeleo ya
Jamii, Viwanda, Uchukuzi, Ujenzi na Tume ya Mipango.
Timu nyingine ni
Mahakama, Tume ya Utumishi wa Umma, Bunge, Tume ya Kurekebisha Sheria,
Tume ya Mahakama, Ukaguzi, tume ya ushirika , Wakala wa Jiolojia
Tanzania, Wakala wa Ukaguzi wa Madini, Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya
Chakula, Mkoa wa Lindi, Katavi, Mwanza, Kagera, Rukwa, Dar es salaam,
Mtwara, Iringa, Geita, Kigoma, Manyara , Arusha, Mara, na Tanga
No comments:
Post a Comment