Jumla ya timu 14 kutoka wilaya ya Arumeru, Mkoani Arusha
,zinachuana vikali katika mashindano ya soka kuwania kombe la
SETHBENJAMINI aliyekuwa muasisi wa Azimio laArusha ambaye alifariki
mwaka 1967.
Timu hizo ni ST.Domingo , Manyata, Duluti,Rafiki, Railway
sports club, Maji ya chai, Embaseni,Usa Star,Meru Worrious, Pande za
home Chemchem, Magadini ,Waya mkali na Chackyi SC zinachuana vikali
katika mashindano
hayo yanayofanyika katika viwanja vya Ngaresero .
Kwa mara ya kwanza mashindano
hayo kufanyika ili kuweza kumkumbuka mwasisi huyo ambaye anakumbukwa
kama shujaa ,alikuwa akisafiri kutoka Arusha kwa matembezi kuelekea Dar
es salaam ambapo alipofika eneo la maji ya chai ,Usa river alizidiwa
gafla na kupoteza maisha papo hapo ilikuwa mwezi julai mwaka 1967 , kwa
mujibu wa diwani wa kata ya Usa River (CCM) Zubery Simbano.
Simbano alieleza kuwa wameamua
kushirikiana na familia ya marehemu ili kuweza kumuenzi katika soka
akiwa yeye ni mmoja wa mashujaa ambao inaonekana wamesahaulika ,hivyo
wataendelea kumuenzi na kumkumbuka kila mwaka .
“ Mashindano haya
yalianzatarehe 22 Julai na tunataraji yatamalizika tarehe 5 septemba
mwaka huu ambapo yata hitimishwa na maandamano kutoka mahali alipozikwa
muasisi huyo, eneo la Laki tatu kanisani hadi eneo la uwanja wa
Ngaresero na maandamano hayo yatahusiha washiriki wote wa
mashindano pamoja na viongozi wa chama cha mapinduzi (CCM) na Viongozi
wa serikali.”alisema Simbano.
Mshindi wa kwanza ataweza
kujinyakulia kitita cha shilingi laki tano (500,000/=) pamoja na
kikombe lenye thamani ya shilingi laki mbili na medali,huku mshindi wa
pili atajipatia seti ya jezi na mipira miwili sambamba na medali,na
mshindi wa tatu atapata mipira 3 na medali.
Pia washiriki wote wataweza
kujipatia vyeti ,na kutakuwa na zawadi mbalimbali kwa mfungaji bora,
mchezaji bora na timu yenye nidhamu vile vile mwisho wa mashindano
kutakuwa na michezo mbalimbali ikiwamo mbio za baiskeli za km 40
zitakazo anzia katika uwanja wa ngaresero hadi Raundi ya Impala na
zitapitia barabara ya Nelson Mandela,kukimbiza kuku, kuvuta kamba .
No comments:
Post a Comment