Dk. Eliud Tongola ambae amekihama chama cha Chadema na kwenda Chama cha ACT -Wazalendo.
.......................................................................
Dar es Salaam. Aliyekuwa mfadhili wa Chadema Jimbo la Musoma Mjini mkoani Mara, Dk Eliud Tongola amejiunga na Chama cha ACT-Wazalendo kinachoongozwa na Zitto Kabwe. Dk Tongola alisema jana kuwa amekuwa mwanachama na mfadhili wa Chadema kwa miaka mitano, lakini amechoshwa na hali inayoendelea katika chama hicho. Alisema hawezi kuvumilia mambo hayo badala yake ameamua kujiengua.
Dk
Tongola alisema sababu iliyomfanya ahamie ACT- Wazalendo ni demokrasia
ya kweli iliyopo katika chama hicho na kwamba, amejipanga kuwatumikia
wakazi wa Musoma Mjini.
“Chadema hakuna demokrasia, ipo kwa watu wachache na wengine wana wagombea wao mifukoni, mfano Julai 3 mwaka huu, Chadema ilitangaza kuwa ni siku ya kuchukua fomu. Mimi na wenzangu tulitekeleza wajibu wetu na kwenda katika ofisi ya chama. “Lakini cha kushangaza tulipofika ofisini tukaambiwa fomu hazipo, hatukukata tamaa tukazitafuta kupitia mitandao na kuzijaza. “Baada ya kujaza tukaambiwa shughuli hiyo imeahirishwa hadi Julai 17 mwaka huu tukakubali,” alidai Dk Tongola. Hata hivyo alisema katika mchakato wa kuchukua na kurudisha fomu za kutangaza nia kugombea ubunge ndani ya Chadema, baadhi ya viongozi walifanya kila jitihada kuhakikisha watu wengine hawashindani na mbunge, Vincent Nyerere. Akizungumzia madai hayo, Nyerere alisema yupo nje ya nchi na kuandika ujumbe unaosema: “Wasiliana na Katibu wa Wilaya na Msimamizi wa Uchaguzi...nilikuwa mgombea kama yeye mwambie tu akuelezea ukweli.” Hata hivyo, Katibu wa Chadema Wilaya ya Musoma Mjini, Hamis Tumbo alisema chama hicho ni taasisi inayoongozwa na kanuni na taratibu zilizowekwa kwa watangazania wote wanaogombea udiwani, ubunge na urais. “Ukibainika umekiuka kanuni za chama unachukuliwa hatua, hivyo Dk Tongola alivunja kanuni,” alisema na kuongeza kuwa mfadhili huyo alikwenda mahakamani ili kusitisha mchakato wa kura za maoni jimboni humo. Ofisa wa Habari wa ACT- Wazalendo, Abdallah Khamis, alisema kuwa Dk Tongola alijiunga wiki mbili zilizopita. Mwananchi. |
August 13, 2015
MFADHILI WA CHADEMA ATIMKIA ACT WAZALENDO
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment