Mkurugenzi wa Sensa ya Watu na Takwimu za Jamii wa Ofisi ya
Taifa ya Takwimu Bw. Ephraimu Kwesigabo akitoa taarifa ya kuongezeka
kidogo kwa mfumuko wa bei nchini kwa mwezi Mei 2015 leo jijini Dar es
salaam.Mfumuko wa Bei wa bei kwa mwezi Julai ,2015 umefikia asilimia
6.4 kutoka asilimia 6.1 iliyokuwepo Juni 2015.
Na. Aron Msigwa – MAELEZO.
11/8/2015. Dar es salaam.
Ofisi ya Taifa ya Takwimu
imetangaza Mfumuko wa Bei wa Taifa kwa mwezi Julai 2015 na kusema kuwa
umeongezeka hadi kufikia asilimia 6.4 kutoka asilimia 6.1 iliyokuwepo
mwezi Juni 2015.
Hii inamaanisha kuwa kasi ya
upandaji wa bei ya bidhaa na huduma kwa mwezi Julai 2015 imeongezeka
ikilinganishwa na kasi ya upandaji bei ya bidhaa na huduma iliyokuwepo
mwezi Juni mwaka 2015.
Mkurugenzi wa Sensa ya Watu na
Takwimu za Jamii wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) Bw. Ephraim
Kwesigabo akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es salaam
amesema kuongezeka huko kumesababishwa na kasi ya upandaji wa bei ya
bidhaa za vyakula na bidhaa zisizo za vyakula katika maeneo mbalimbali
nchini.
Amezitaja bidhaa za vyakula
zilizochangia kuongezeka kwa mfumuko huo kutokana na upandaji wa bei
katika masoko kwa mwezi Julai 2015 kuwa ni mchele kwa asilimia
27.9,mahindi asilimia 2.3, unga wa muhogo asilimia 9.2, nyama asilimia
4.5, samaki 12.2, na maharage asilimia 5.9.
Kuhusu Fahirisi za Bei ambacho
ni kipimo kinachotumika kupima mabadiliko ya bei ya bidhaa na huduma
zinazotumiwa na kaya binafsi hapa Tanzania, Kwesigabo amesema
zimeongezeka hadi kufikia 158.78 kutoka 158:12 za mwezi Juni.
Amesema kuongezeka kwa fahirisi
za bei kumechangiwa na ongezeko la bei ya baadhi ya bidhaa za vyakula
na bidhaa zisizo za vyakula zikiwemo gesi ya kupikia kwa asilimia 3.7,
mafuta ya dizeli 5.9, mafuta ya Petroli ailimia 4.9, unga wa mahindi
asilimia 2.5, ulezi asilimia 2.9, samaki asilimia 4.8, viazi vitamu
asilimia 2.6 na ndizi za kupika asilimia 3.4.
|
August 11, 2015
MFUMUKO WA BEI WA TAIFA WAONGEZEKA
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment