Miss Tanzania 2012, Brigite Alfred akizindua ujenzi wa bweni la Albino Buhangija mkoani Shinyanga. |
Miss Tanzania 2012, Brigite Alfred akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya Albino mara baada ya kuzindua mafunzo ya Ujasiriamali Makumbusho ya Taifa. |
……………………………………………………………………………………….
Taasisi ya Miss Tanzania 2012,
Brigitte Alfred Foundation (BAF) kwa kushirikiana na Taasisi ya Junior
Achievement (JA) imeendeleza zoezi la kutoa mafunzo ya Ujasiriamali kwa
wajamii ya watu wenye albino nchini.
Mafunzo hayo ya wiki mbili
yalifunguliwa na mkuu wa mkoa wa Kigoma ambapo jumla ya albino 20
walifaidika na mafunzo hayo yaliyozinduliwa na mkuu wa mkoa wa Kigoma,
kanali mstaafu Issa Machibya. Mbali ya watu wenye albino, washiriki
wengine katika mafunzo hayo walikuwa wanawake na vijana.
Machibya alitoa wito kwa
taaisis nyingine kuiga mfano taasisi ya Brigitte na Junior Achievements
ambayo mpaka sasa imetoa mafunzo kama hayo kwa vijana na akina mama
25,000.
Mkuu wa mkoa huyo alisema kuwa
mafunzo ya ujasiliamari ni muhimu kwa kila mtu na kupongeza juhudi za
mrembo huyo ambaye mpaka sasa ametoa mafunzo kwa watu wenye albino 70.
Kati ya hao 70, albino 50 walipata mafunzo jijini Dar es Salaam.
“Haya ndiyo mambo muhimu ya
kuigwa kwa jamii, taasisi ya Brigite imetoa elimu ambayo itawawezesha
wahitimu kufanyakazi ya ujasiriamali na kujipatia kipato kwa jasho lako,
nawapongeza sana na taasisi nyingine zifuate nyayo,” alisema Mashibya.
Mratibu wa mafunzo hayo,
Stanley Mosha alisema kuwa kwa kupitia BAF kwa sasa unaende vizuri na
lengo lao ni kutoa mafunzo kwa watu wenye albino kila mkoa na wamepanga
kutoa mafunzo kwa albino 300 nchi nzima kwa mwaka 2015.
Mosha alisema kuwa lengo lao
mafunzo hayo ni kuwawezesha kiuchumi vikundimbalimbali hususani vijana
na wakinamama. Alisema kuwa hatua hiyo imetokana na mafanikio ya
Brigitte katika mashindano ya urembo ya Dunia ya mwaka 2013 nchini
Indonesia na kushika nafasi ya tatu kupitia taji la mrembo mwenye
malengo baada ya kuonyesha dunia jitihada zake za kusaidia watu wenye
ualbino nchini Tanzania.
Alisema kuwa kuanzia hapo,
Brigitte amekuwa Balozi wa watu kwa watu wenye ualbino Tanzania na
kufanya shughuli mbalimbali za kuwasaidia mfano ujenzi wa bweni la
kisasa lenye uwezo wa kuchukua idadi ya watoto 60, na uboreshaji
mazingira kituo cha Buhangija mkoani Shinyanga.
“Nimefuraishwa na Mwitikio na
ushirikiano walioonyesha kwa kutambua na kukubali kuliingiza kundi hili
na kuweza kuungana na makundi mengine ya vijana katika program za
ujasiriamali. Kulitambua na kulijumuisha kundi hili katika kuwajengea
uwezo ni hatua kubwa inayowezesha kupanua wigo na juhudi za kuwezesha
makundi ya vijana na wakinamama kiuchumi na tunaomba wadau wengine
waungane nasi katika hili,” alisema Mosha.
Kwa upande wake, Brigitte
alisema kuwa ataendeleza mpango huo hapa nchini na anaamini atafikia
lengo lake. “Nashukuru Junior Achievement kwa kuniunga mkono katika
mpango huu ambao kwa sasa unapata mafanikio makubwa, naomba kuungwa
mkono kwani jukumu hili ni la watanzania wote,” alisema Brigitte.
No comments:
Post a Comment