Mwamoto akionyesha fomu ya ubunge kulia kwake ni dada wa prof Peter Msolla Anna Msola na kutoka kulia ni msimamizi mkuu wa uchaguzi Lukia Mhango na Msaidizi wake |
Na MatukiodaimaBlog ,Kilolo
Mgombea mteule ubunge CCM jimbo la Kilolo Venance Mwamoto ametangaza msahama kwa wajumbe wa kamati ya siasa na wagombea udiwani ambao walikuwa upande wa mbunge wa zamani Prof Peter Msolla huku akiwataka kupenda ili kuwezesha jimbo hilo kupiga hatua ya kimaendeleo
Mwamoto alisema kuwa hana kinyongo na mgombea yeyeto Kati ya wagombea 15 waliojitokeza na kumwomba prof Msola kuonyesha ushirikiano katika kampeni ili kuwezesha ushindi kwa Mgombea urais wa Ccm Dr John Magufuli, ubunge na Madiwani wote wa CCM.
Mwamoto ametoa kauli hiyo Mchana wa leo wakati akitoa kuchukua fomu ya ubunge na kuwawapongeza wagombea hao wa ccm udiwani kwa kuteuliwa huku akiahidi kuwapa ushirikiano mkubwa katika kata zao ikiwa ni pamoja na kuhakikisha mabango Yake yanakuwa na picha ya diwani kwa kata husika .
Kwani alisema haipendezi kuona makundi ya kampeni z kura za maoni yanaendelea katika jimbo na kata za jimbo la Kilolo.
Hivyo aliwataka wagombea hao wa udiwani kuandika barua za kuwapongeza kwa kushiriki kura za maoni wale wote waliogombea nao pamoja na kuwaomba kushiriki kampeni badala ya kuwabagua na kujigamba kwa kushinda.
Alisema jimbo hilo ili lipige hatua katika maendeleo linahitaji umoja zaidi toka kwa mabalozi, wenyeviti, Madiwani na mbunge
Huku akiwataka Madiwani hao baada ya kushinda kutokwenda katika vikao vya madiwani bila kufanya mikutano na wananchi
"Ni marufuku kwa diwani hata Mimi mbunge kwenda bungeni bila ya kuchukua kero za wananchi kwenda bungeni ama katika mabaraza ya Madiwani bila kukutana na wananchi si uwakilishi unaotakiwa,"
Mwamoto alisema kuwa jimbo hilo la Kilolo anataka liwe jimbo la mfano kwa maendeleo katika Mkoa wa Iringa hivyo Kazi Yake kubwa kwa sasa ni
kuhakikisha anabainisha changamoto zote na kuanza na chache katika
utekelezaji .
kuhakikisha anabainisha changamoto zote na kuanza na chache katika
utekelezaji .
Alisema zipo changamoto sugu katika jimbo hilo ikiwemo ya maji katika mji wa Ilula ambayo ataanza kuitatua mapema pia shamba la chai Kidabaga kwa kuona mwekezaji anapatikana ama kurudi kwa wananchi .
Huku Mgombea mteule wa udiwani kata ya Ilula Anna Msolla akizungumza kwa niaba ya wagombea udiwani jimbo la kilolo waliomsindikiza Mwamoto
kuchukua fomu alisema kuwa kuteuliwa kwa Mwamoto kuwa Mgombea ubunge kilolo ni ushindi wa kishindo kwa ccm jimbo hilo na ushindi wa Madiwani na Mgombea urais Dr Magufuli .
kuchukua fomu alisema kuwa kuteuliwa kwa Mwamoto kuwa Mgombea ubunge kilolo ni ushindi wa kishindo kwa ccm jimbo hilo na ushindi wa Madiwani na Mgombea urais Dr Magufuli .
Msimamizi mkuu wa uchaguzi jimbo la Kilolo Lukia Mhango alisema kuwa jumla ya vyama vitatu vimechukua fomu ya ubunge kikiwemo chama cha mapinduzi, Chausta na ACT wazalendo huku akisema ruksa kwa wagombea kuchukua na kurejesha fomu kwa shamla shamla .
No comments:
Post a Comment