……………………………………………………………………..
Na.Aron Msigwa – MAELEZO.
ARUSHA
Matumizi ya Teknolojia ya
Habari na Mawasiliano katika ukusanyaji wa mapato ya Serikali
yamepunguza upotevu wa mapato uliokuwa ukisababishwa na watendaji wasio
waaminifu.
Kauli hiyo imetolewa jana
jijini Arusha na Katibu Tawala wa Mkoa wa Arusha Bw. Adorf Mapunda
wakati akifunga awamu ya kwanza ya mkutano wa mwaka wa Serikali Mtandao
uliowahusisha maafisa TEHAMA,Rasilimali watu,Utawala na Maafisa Habari
kutoka maeneo mbalimbali nchini.
Amesema mabadiliko hayo ya
ukusanyaji wa fedha kielektroniki yameongeza ufanisi kwa kuongeza
ukusanyaji wa mapato na kuondoa wizi na vitendo vya rushwa vilivyokuwa
vikifanywa na baadhi ya watumishi wa Serikali wasio waaminifu.
Ameeleza kuwa utendaji wa Serikali na taasisi zake umerahisishwa kupitia Teknolojia ya Habari na Mawasiliano.
No comments:
Post a Comment