Wauguzi wakiwa katika wodi iliyotengwa kwa ajili ya
kuwahudumia wagonjwa wenye dalili za kipindupindu katika Hospitali ya
Mwananyamala, Dar es Salaam, jana. Picha na Salim Shao
UGONJWA wa kipindupindu umezidi kushika kasi mkoani Dar es Salaam, baada ya idadi ya wagonjwa kuongezeka kutoka 27 hadi 34.
Akizungumza na MTANZANIA mjini Dar es Salaama jana, Mratibu wa Huduma
za Dharura, Mkoa wa Dar es Salaam, Victoria Bura alisema kumekuwapo na
ongezeko la ugonjwa huo katika Wilaya ya Kinondoni.
Alitaja maeneo yaliyoathirika na ugonjwa huo kuwa ni Kijitonyama, Makumbusho, Saranga, Manzese, Tandale, Kimara na Mwananyamala.
Kwa mujibu wa Bura, wagonjwa watatu kati ya hao wamefariki dunia na wengine wane wameruhusiwa baada ya afya zao kuimarika.
“Kumekuwapo na ongezeko la wagonjwa wapya saba, hali hii inaonyesha tatizo lipo katika maeneo hayo niliyotaja.
“Takwimu zetu, zinaonesha hatuja pokea taarifa zozote kutoka wilaya
za Ilala na Temeke, nawaomba wakazi wa maeno mengine kuchukua hadhari
kwa kuzingatia kanuni za usafi na kuepuka mikusanyiko ya watu isiyo ya
lazima,”alisema.
Kutokana na hali hiyo, Bura aliwataka wananchi kufanya usafi katika
maeneo yao na hasa majumbani na wafanyabiashara kama vile wauza
matunda na mama lishe.
“Ili kufanikiwa kudhibiti ugonjwa huu, tunaziomba serikali za mitaa
zisimamia jambo nyumba kwa nyumba, maana tunaamini wao ndiyo wako karibu
zaidi na wananchi,”alisema Bura.
Kuhusu mgonjwa aliyefariki, alisema alifikishwa hospitalini akiwa
anatapika na kuharisha dalili ambayo iliyoonesha kuwa amepatwa na
ugonjwa huo.
Alisema familia yake nayo ilikuwa imepatwa na dalili ya ya ugonjwa huo.
“Jumamosi saa 2:00 asubuhi Hospitali ya Mwananyamala ilipokea
mgongwa mwanamume mwenye umri wa miaka 50, akiwa amefariki dunia
kutokana na kuharisha na kutapika akitokea mtaa wa Ally Maua,
Kijitonyama.
“Baada ya kufuatilia kwa kina,tulichukua hatua haraka kwa kutoa
huduma kwa familia na kunyunyuzia dawa ya kuua vijidudu kwenye
maji,”alisema.
Naye Mganga Mkuu wa Jiji la Dar es Salaam, Judithi Kahama alisema
tayari kambi ya madaktari imewekwa katika hospitali za Sinza na
Mwananyala ili kutoa huduma zinazohitajika kwa wagonjwa.
Alisema kambi nyingine, zimewekwa katika Hospitali ya Mburahati,
Buguruni na Temeke, huku zote zikiwa na dawa za kutosha za kukabiliana
na ugonjwa huo.
|
August 19, 2015
WATU 34 HOI KWA KIPINDUPINDU DAR
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment