Na Mwandishi Wetu
MIKOA 10 ya Tanzania bara, Inatarajia kuombea amani na utulivu katika Uchaguzi Mkuu unaotarajia kufanyika Oktoba 25 mwaka huu hapa nchini. Kwa mujibu wa Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Msama Promotions, Alex Msama mikoa hiyo itaiombea amani Tanzania kupitia muziki wa Injili kupitia waimbaji mbalimbali wa ndani na nje ya nchi. Msama alisema awali kabla ya mikoa hiyo kuombea amani uchaguzi Mkuu, Tamasha la kwanza lenye dhamira hiyo litafanyika Oktoba 4 jijini Dar es Salaam. “Tumeona kuna umuhimu kuwashirikisha waimbaji wa nyimbo za Injili kumuomba Mungu atuongoze katika uchaguzi Mkuu ambao unatakiwa kuwa huru na haki, ili kufanikisha hayo kwa ufanisi nyimbo za kumuomba na kumtukuza Mungu zitumike ili dua na sala zisikike mbinguni,” alisema Msama. Msama alisema Kamati yake bado inaendelea na mchakato wa kufanikisha maandalizi ya tamasha hilo ambalo litaimarisha na kudumisha amani na utulivu ulioasisiwa na baba wa Taifa Mwalim Julius Kambarage Nyerere. Aidha Msama alisema tamasha hilo litashirikisha waimbaji mbalimbali wakiwemo wa Tanzania na nje ambao watasaidia kufikisha ujumbe huo kwa Mungu. Msama alisema wananchi wajiandae kupata neno la Mungu kupitia waimbaji wa nyimbo za Injili ambao watafanikisha mungu kusikia wanachohitaji wananchi. |
August 19, 2015
MIKOA 10 KUOMBEA UCHAGUZI MKUU
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment