KWA MAONI AU USHAURI E-mail: inocomm2014@gmail.com, PIGA SIMU: 0714555668

www.utt-pid.org


TEMBELEA: www.utt-pid.org

August 9, 2015

OFISI YA WAZIRI MKUU YAIBUKA MSHINDI WA KWANZA KWA WIZARA ZA HUDUMA ZA JAMII KATIKA MAONESHO YA NANE NANE KITAIFA – LINDI

mak1
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Jakaya Kikwete akimpongeza Mkurugenzi Idara ya Uratibu wa maafa Ofisi ya Waziri Mkuu, Brigedia Jenerali, Mbazi  Msuya kwa ofisi hiyo kuwa mshindi wa kwanza kwa Wizara za Huduma za Jamii zilizoshiriki maonesho ya Nane Nane Kitaifa mkoani Lindi, Tarehe 8 Agosti, 2015.
mak2
Baadhi ya watumishi wa Ofisi ya Waziri Mkuu wakifurahia  kombe la kuwa mshindi wa kwanza kwa Wizara za Huduma za Jamii zilizoshiriki maonesho ya Nane Nane Kitaifa mkoani Lindi, Tarehe 8 Agosti , 2015, walioshika kombe hilo katikati ni Mkurugenzi Idara ya Uratibu wa maafa Ofisi ya Waziri Mkuu, Brigedia Jenerali, Mbazi Msuya, kulia kwake ni Msajili wa vyama vya siasa, Jaji Francis Mutungi na kushoto kwake ni Mkurugenzi Idara ya Uratibu Maadhimisho ya Kitaifa  Ofisi ya Waziri Mkuu, Flora Mazilengwe.
mak3
Msajili wa vyama vya siasa, Jaji Francis Mutungi  akipata maelezo ya bidhaa zinazotengezwa na vikundi vya wajasiriamali kutoka Zanzibar waliowezeshwa na Ofisi ya Waziri Mkuu kupitia Programu ya Miundo Mbinu ya Masoko, Uongezaji Thamani na Huduma za Kifedha Vijijini (MIVARF) na kushoto kwake ni Mkurugenzi Idara ya Uratibu Maadhimisho ya Kitaifa  Ofisi ya Waziri Mkuu, Flora Mazilengwe, walipotembelea banda hilo Tarehe 8 Agosti , 2015.                                

No comments:

Post a Comment