Na Lorietha Laurence-Maelezo
Bodi ya Mfuko wa Barabara
nchini(RFB) imefanikiwa kufanya maboresha ya barabara kwa kiwango cha
lami katika kipindi cha miaka kumi ya uongozi wa Serikali ya awamu ya
nne wa Mhe. Jakaya Kikwete.
Akizungumza na waandishi wa
habari Dar es Salaam Jana Bw. Joseph Haule amesema kuwa matengenezo
hayo yamefanikisha ujenzi wa barabara kuu zinazounganisha mikoa
mbalimbali nchini kukamilika kwa asilimia 89 huku zile za Wilaya na Miji
kwa asilimia 57.
“ kazi kubwa ya Mfuko huu ni
kukusanya mapato kupitia vyanzo mbalimbali ikiwemo tozo za barabarani
na ushuru wa mafuta na baadaye kuzigawa kupitia taasisi zinazohusika
na ujenzi wa barabara ikiwemo TANROADS, Wizara ya Ujenzi na Ofisi ya
Waziri Mkuu “ alisema Bw. Haule
Aidha aliongeza kuwa Mfuko huo
umefanikisha ujenzi wa daraja la Mabatini jijini Mwanza ,daraja la
Mwanhunzi na daraja la Mbutu linalounganisha Igunga na Shinyanga
pamoja na ununuzi wa vivuko kikiwemo kile cha Mv Malagarasi.
Mbali na hayo Bw.Haule aliongeza
kuwa Bodi hiyo inaendelea kuhakikisha barabara zinatunzwa kwa
kudhibiti magari ya mizigo yanayozidisha uzito unaochangia uharibifu wa
barabara kwa kuanzisha mfumo wa kisasa wa kamera utakaokuwa
unaratibiwa na mfuko huo.
Mfuko huo umefanikiwa kuanzisha
ujenzi wa barabara kwa kutumia mawe ambao ni wa gharama nafuu na wa
kudumu kwa muda mrefu,hata hivyo miradi hiyo imeanza kutekeleza katika
mikoa ya Kigoma na Mwanza.
Kutokana na mtandao wa barabara
kufanyiwa matengenezo ya mara kwa mara imesaidia kuongeza ubora wa
barabara na kupanua wigo wa biashara kati ya Tanzania na nchi za jirani
ikiwemo Zambia,Malawi,Burundi,Rwanda na Uganda.
Mbali na mafanikio hayo Mfuko
huounakabiliana na changamoto mbalimbali ikiwemo upungufu wa bajeti
kutokana na fedha zinazopatikana kutokukidhi mahitaji.
No comments:
Post a Comment