MWENDESHA PIKIPIKI @ BODABODA
ALIYEFAHAMIKA KWA JINA LA BAHATI MAHELA (23) MKAZI WA SAE ALIFARIKI
DUNIA WAKATI ANAPATIWA MATIBABU HOSPITALI YA RUFAA JIJINI MBEYA BAADA YA
KUCHOMWA KISU SHINGONI.
TUKIO HILO LIMETOKEA MNAMO TAREHE 10.08.2015 MAJIRA YA SAA 20:00 USIKU HUKO ENEO LA ITUHA BAADA YA MAREHEMU KUKODISHWA NA ABIRIA ASIYEMFAHAMU KUTOKA KIJIWE CHA SAE KWENDA SHULE YA MSINGI ITUHA NA NDIPO WAKIWA NJIANI ALICHOMWA KISU SHINGONI NA KISHA KUMPORA PIKIPIKI YAKE YENYE NAMBA ZA USAJILI MC 851 ABG AINA YA KINGLION.
KUFUATIA TUKIO HILO MSAKO
UMEFANYIKA NA PIKIPIKI IMEPATIKANA IKIWA IMETELEKEZWA ENEO LA UYOLE.
CHANZO CHA KIFO CHAKE NI KUTOKWA DAMU NYINGI BAADA YA KUCHOMWA KISU
SHINGONI NA KIINI CHA TUKIO HILI NI KUWANIA MALI.
MWILI WA MAREHEMU
UMEHIFADHIWA HOSPITALI YA RUFAA MBEYA. UPELELEZI UNAENDELEA IKIWA NI
PAMOJA NA KUMTAFUTA ALIYEHUSIKA KATIKA TUKIO HILI.
TAARIFA ZA MSAKO:
KATIKA MSAKO WA KWANZA,
WATU WANNE WOTE WAKAZI WA KIJIJI CHA NAMOLE WILAYA YA MOMBA
WALIOFAHAMIKA KWA MAJINA YA 1. ALLY ANSISYE (24) 2. ALIKWA SIYAME (25)
3. SAMWEL KAMINYOGE (32) NA 4. FATUMA D/O ANANGISYE (30) WAKIWA NA POMBE
HARAMU YA MOSHI [GONGO] UJAZO WA LITA NNE (04).
WATUHUMIWA WALIKAMATWA KATIKA
MSAKO ULIOFANYIKA MNAMO TAREHE 11.08.2015 MAJIRA YA SAA 12:00 MCHANA
HUKO KATIKA KIJIJI CHA NAMOLE, KATA YA CHIWEZI, TARAFA YA TUNDUMA,
WILAYA YA MOMBA, MKOA WA MBEYA.
KATIKA MSAKO WA PILI,
MTU MMOJA MKAZI WA MPEMBA WILAYA YA MOMBA ALIYEFAHAMIKA KWA JINA LA
DANIEL SAMSON MNOZYA (32) ANASHIKILIWA NA JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA
AKIWA NA BHANGI UZITO WA KILO TATU (03).
MTUHUMIWA ALIKAMATWA MNAMO TAREHE
11.08.2015 MAJIRA YA SAA 12:00 MCHANA HUKO KATIKA ENEO LA MPEMBA, KATA
YA CHIWEZI, TARAFA YA TUNDUMA, WILAYA YA MOMBA, MKOA WA MBEYA.
TARATIBU ZA KUWAFIKISHA WATUHUMIWA MAHAKAMANI ZINAENDELEA.
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA
KAMISHNA MSAIDIZI MWANDAMIZI WA POLISI AHMED Z. MSANGI ANATOA YEYOTE
MWENYE TAARIFA ZA MTU ALIYEHUSIKA KATIKA TUKIO LA MAUAJI YA MWENDESHA
PIKIPIKI AZITOE KATIKA MAMLAKA HUSIKA ILI AKAMATWE NA HATUA ZA KISHERIA
ZICHUKULIWE DHIDI YAKE.
AIDHA ANAENDELEA KUTOA WITO KWA JAMII KUACHA
KUTUMIA DAWA ZA KULEVYA NA POMBE HARAMU YA MOSHI [GONGO] KWANI NI
KINYUME CHA SHERIA NA NI HATARI KWA AFYA YA MTUMIAJI.
Imesainiwa na:
[AHMED Z. MSANGI – SACP]
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA.
No comments:
Post a Comment