Wasanii wakipata maelekezo kutoka kwa Mwenyekiti wa SHIWATA, Cassim Taalib (hayupo pichani) utaratibu wa kutunza nyumba walizogaiwa kwenye kijiji cha Wasanii Mwanzega, Mkuranga juzi . |
Mwenyekiti wa SHIWATA, Cassim Taalib akitoa ufafanuzi wa makazi mapya ya kijiji cha M\Wasanii Mwanzega, Mkuranga baada ya kugawa nyumba 16 kwa wasanii hao. |
Wasanii wa Shiwata wakifurahia picha ya pamoja baada ya kukabidhiwa nyumba katika kijiji cha wasanii, Mkuranga |
……………………………………………………………………………………
MTANDAO wa Wasanii Tanzania
(SHIWATA) imegawa nyumba nyingine 16 kwa wanachama wake waliokamilisha
ujenzi ambako mpaka sasa wanachama 120 wamekabidhiwa nyumba zao katika
kijiji cha Wasanii cha Mwanzega, Mkuranga.
Katika hafla ya kukabidhi nyumba
hizo jana, Mwenyekiti wa SHIWATA, Cassim Taalib alisema mpango wa ujenzi
wa nyumba hizo ni endelevu mpaka hapo ekari 300 zilizotengwa kwa ujenzi
zitajengwa nyumba kwa mpango wa kuchangiana.
Taalib alisema aina za nyumba
zinazojengwa kwa sasa ni za matofali ya saruji ya chuma kimoja kwa sh.
750,000, nyumba za vyumba viwili na sebule kwa sh. 3.8 na nyumba kubwa
ya sh. mil. 6.4.
Alisema kipa wa zamani wa Yanga
na timu ya Taifa, Hamisi Kinye anatarajia kukabidhiwa nyumba yake
Desemba mwaka huu sambamba na wasanii wengine Lilian Ndelwa, Edson
Mwela, Happyness Magere, Asheri Kazeba, Jaqueline Joseph na Suzan Moshi
ambao wamebadilisha nyumba walizokuwa wakabidhiwe za udongo na sasa
watachukua nyumba zilizojengwa kwa saruji.
Mwenyekiti Taalib alisema SHIWATA
imeandaa mpango mkakati wa kuingiza umeme na maji katika kijiji hicho
kabla ya Desemba na tayari kikundi cha wasanii kimepiga kambi ya
kujiandaa kurekodi tamthilia ya maisha ya Bongo katika kijiji hicho.
Mmoja wa wasanii aliyekabidhiwa
nyumba ya sh. mil. 6.4, Mwajuma Kisengo alisema ametimiza ndoto yake ya
kushirikiana na wasanii wenzake kuishi katika kijiji cha Mwanzega,
Mkuranga.
No comments:
Post a Comment