Shirikisho
la Mpira wa Miguu nchini Tanzania (TFF) limesaini mkataba mpya wa miaka mitatu
(3) wa udhamini wa Ligi Kuu Tanzania bara (VPL) wenye thamani ya shilingi
bilioni sita (tsh bilioni 6.6) na kampuni ya simu ya Vodacom, halfa hiyo imefanyika
leo katika ofisi za makao makuu ya kampuni hiyo eneo la Mlimani City jijini Dar
es salaam.
Akiongea
wakati wa kusaini mktaba huo mpya, Mkurugenzi wa masoko wa kampuni ya simu ya
Vodacom Kelvin Twissa, amesema kampuni yao inafurahia kuendelea kuwa sehemu ya udhamini
ya ligi kuu nchini, mafanikio ya timu bora na kufanya vizuri katika michuano ya
kimataifa inatokana na kuwa na ligi bora ambayo inadhaminiwa na Vodacom.
Naye
Rais wa TFF, Jamal Malinzi amewashukuru kampuni ya Vodacom kwa kukubali
kuendelea kuidhamini ligi kuu kwa kipindi kingine cha miaka mitatu (3) na
kuongeza sehemuya udhamini wao kwa asilimia 40%.
Tunaishukuru
kampuni ya Vodacom kwa kuendelea kuwa sehemu ya mafanikio ya mpira wa miguu
nchini, udhamini wanaotupatia unavisaidia vilabu kujiandaa na kujiendesha na
mikikimikiki ya ligi na kuifanya ligi kuwa na ushindani wa hali ya juu, msimu
huu ligi itakua na timu 16 tunatarajia kuendelea kushuhudia uhondo huo chini ya
udhamini wa kampuni ya simu za mkononi ya Vodacom.
Mkataba
huo mpya wa udhamini kwa kipindi cha miaka mitatu, umeboreshwa na kuwa na
ongezeko la asilimia 40% kutoka katika mkataba wa awali uliomalizika.
Ligi
Kuu ya Vodacom inatarajiwa kuanza kutimua vumbi Septemba 12, 2015.
TFF YAMPONGEZA JAJI MAMBI
Rais
wa Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini (TFF), Jamal Malinzi amempongeza Makamu
Mwenyekiti wa Kamati ya Uchaguzi ya TFF, Adam Mambi kwa kuteuliwa kuwa Jaji wa
Mahakama Kuu nchini.
Katika
Salam zake kwa Jaji Mambi, Malinzi amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania, Dokta Jakaya Kikwete kwa kumteua mwanafamilia huyo wa mpira wa miguu
nchini kushika wadhifa huo.
TFF
kwa niaba ya familia ya mpira wa miguu na watanzania wote inamtakia kila la kheri
Jaji Adam Mambi katika majukumu yake mapya ya Ujaji katika Mahakama Kuu nchini
Tanzania.
TRA KUENDESHA SEMINA YA KODI
Mamlaka
ya Kodi na Mapato nchini (TRA) inatarajiwa kuendesha semina ya kodi kwa
viongozi wa vilabu viliyopo jijini Dar es salaam, siku ya ijumaa tarehe 14
Agosti katika hoteli ya Tiffany iliyopo eneo la Kisutu.
TRA
itaendesha semina hiyo kwa vilabu vilivyopo ligi kuu, ligi daraja la kwanza na
ligi daraja la pili ambapo viongozi wakuu wa vilabu hivyo, Katibu Mkuu,
Mwenyekiti, na Mhasibu wanapaswa kuhudhuria semina hiyo.
Kwa
kuanzia TRA itaendesha semina hiyo jijini Dar es salaa, na baadae kuendelea na
semina hizo kwa vilabu vilivyopo mikoani kwa lengo la viongozi wa vilabu
kutambua umuhimu wa ulipaji kodi kwa wachezaji, makocha wanaowaajiri katika
vilabu vyao.
Semina
hiyo itaanza saa 3 asubuhi mpaka saa 5 kamili asubuhi katika hoteli ya Tiffany
iliyopo eneo la Kisutu jijini Dar es salaam, vionggozi wa vilabu vya ligi kuu,
ligi daraja la kwanza, ligi daraja la pili waliopo jijini Dar es salaam
mnaombwa kuhudhuria semina hiyo.
IMETOLEWA
NA SHIRIKISHO LA MPIRA WA MIGUU TANZANIA (TFF)
No comments:
Post a Comment