TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Ofisi ya Makamu wa Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, inasikitika kuwepo kwa taarifa za
uzushi ambazo zimesambaaa kwenye mitandao ya kijamii zinazodai kuwa
Mheshimiwa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.
Mohammed Gharib Bilal ataongea na vyombo vya habari kuhusu msimamo wake
ndani ya Serikali na Chama Cha Mapinduzi.
Habari hizi si za kweli na
tunaomba kuueleza umma wa Watanzania kuwa
Mheshimiwa Makamu wa Rais,
hausiki na taarifa hizo zilizoenea kwenye mitandao ya Kijamii na wala
hajapanga tukio lolote la kukutana na waandishi wa habari na wala hana
mpango wa kuzungumzia msimamo wake ndani ya Serikali na Chama Cha
Mapinduzi.
Aidha tunatumia nafasi hii
kuwataka wale wote wenye tabia ya kuvumisha taarifa zisizo sahihi kwa
maslahi yao waache kufanya hivyo kwa kuwa ni kosa kisheria.
Tunawaomba
waandishi wa habari kufuata taratibu za kazi na kutafuta taarifa sahihi
kwenye vyombo vinavyohusika na kutambulika.
Boniphace Makene
Mwandishi wa Habari wa Makamu wa Rais
10/8/2015
No comments:
Post a Comment