KWA MAONI AU USHAURI E-mail: inocomm2014@gmail.com, PIGA SIMU: 0714555668

www.utt-pid.org


TEMBELEA: www.utt-pid.org

August 15, 2015

TAREHE 15 AGOSTI 2015 MALINZI AMPONGEZA NDIKURIYO

Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini (TFF), Jamal Malinzi ametuma salamu za pongezi kwa Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini Burundi (FBF) Reverien Ndikuriyo kwa kuchaguliwa kuwa spika wa bunge la Seneta nchini humo.

Katika salam hizo za pongezi kwa Rais wa FBF na nakala zake kwenda CECAFA, CAF na FIFA, Malinzi ameelezea imani yake kwa Seneta Ndikuriyo na amemtakia kila la kheri na mafanikio katika nafasi hiyo mpya aliyochaguliwa.


TWIGA STARS YAENDELEA KUJIFUA ZANZIBAR
Kikosi cha timu ya Taifa ya Wanawake (Twiga Stars) kilichoweka kambi kisiwani Zanzibar, kujiandaa na fainali za Michezo ya Afrika (All Africa Games) kimeendelea kujifua kutwa mara mbili katika viwanja wa Aman na Fuoni kabla ya safari ya kuelekea nchini Congo – Brazzavile mwezi ujao.

Twiga Stars chini ya kocha mkuu Rogasian Kaijage inatarajiwa kucheza mchezo wa kirafiki na timu ya Taifa ya Kenya (Harambee Starlets) Agosti 23  katika uwanja wa Amani kisiwani Zanzibari ikiwa ni sehemu ya maandalizi ya michezo ya hiyo ya Afrika (All Africa Games).

Kaijage amesema anashukru vijana wake wanafanya mazoezi kwa morali ya hali ya juu, wachezaji wanaonekana kuyashika vizuri mafunzo yake na kumpa imani kuwa sasa kikosi chake kimeiva na anachosubiri ni mchezo wa kirafiki dhidi ya Kenya ili kuweza kuona uwezo wa kikosi chake kabla ya safari ya kuelekea nchini Congo-Brazzavile.

Akiongeleaa maendeleo ya kambi ya Twiga Stars, Mkuu wa Msafara Blassy Kiondo amesema timu ipo katika hali nzuri, wachezaji wanafanya mazoezi  kwa morali ya hali ya juu, hakuna majeruhi kikubwa wanachosubiri kwa sasa ni huo mchezo wa kirafiki dhidi ya Kenya mwishoni mwa wiki ijayo.

IMETOLEWA NA SHIRIKISHO LA MPIRA WA MIGUU TANZANIA (TFF)

No comments:

Post a Comment