Waziri wa Nishati na Madini, George Simbachawene amesema
umeme wa gesi utaanza kutumika mwezi ujao baada ya ujenzi wa bomba la kupitisha
gesi hiyo kukamilika kwa asilimia 100.
Akizungumza juzi wakati alipotembelea mradi wa ujenzi wa
bomba hilo na mitambo ya umeme wa Kinyerezi, Simbachawene alisema bomba hilo
limekamilika na liko kwenye hatua ya majaribio.
Alisema hatua
mbalimbali za majaribio zilianza tangu Julai 24, mwaka huu na kazi inayofanyika
sasa ni majaribio ya kuunganishwa bomba hilo na njia kuu ya umeme ya msongo wa
kilovoti 220 wenye urefu wa kilomita nane kutoka kituo cha kupozea umeme cha
Kinyerezi hadi Kimara.
“Nafahamu kwa siku za
karibuni hali ya umeme katika baadhi ya mikoa siyo nzuri, nawaomba wananchi
wawe wavumilivu, kwani tatizo hilo liko katika hatua za mwisho kumalizika,”
alisema. Simbachawene.
Alisema gesi hiyo kabla haijaanza kutumika yatafanyika
majaribio, ikiwamo mitambo ya kuchakata gesi, usafirishaji wa gesi, uwashwaji
wa mitambo ya kufua umeme, uunganishaji wa laini ya umeme utakaozalishwa kutoka
mitambo ya Ubungo na majaribio ya kusafirisha umeme kutoka katika mtambo wa
Kinyerezi kwenda Gridi ya Taifa.
Simbachawene alisema Shirika la Maendeleo ya Petroli (TPDC)
lilianza kazi ya upimaji wa mtambo wa Madimba kuhimili kiwango cha gesi
inayoingia na kuichakata katika viwango vinavyotakiwa kwa muda wa wiki mbili.
Mkurugenzi Mkuu wa TPDC, Dk James Mataragio alisema
walishaanza kutoa gesi ardhini na kuipeleka kwenye Mtambo wa Madimba kabla
kuisafirisha kwenda Kinyerezi.
Mkurugenzi Mtendaji wa Tanesco, Felchesmi Mramba alisema
mitambo ipo kwenye majaribio, hivyo watalazimika kukata mitambo ya kituo cha
Ubungo, Tegeta na Kinyerezi kwa nyakati tofauti wakati wa kuunganisha umeme wa
gesi.
|
August 10, 2015
UMEME WA GESI SASA KUANZA MWEZI UJAO
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment