![]() |
Afisa Masoko UTT-PID, Bi Kilave Atenaka akihudumia mteja katika banda lao lililo chini ya wizara ya Fedha katika Maonesho ya Nane Nane yanayoendelea katika viwanja vya Ngongo mkoani Lindi. |
Muonekano wa viwanja vya Mabano vilivyopimwa na Taasisi ya UTT-PID kwa ushirikiano na Halmashauri vilivyopo Manispaa ya Lindi. |
Zaidi
ya viwanja 2,500 vilipimwa kwa ajili ya matumizi mbalimbali kama vile
Makazi, Biashara, Maeneo ya Umma na sehemu za kupumzika.
Akielezea
Afisa Masoko Bi. Kilave Atenaka alisema kuwa kwa sasa wanaendesha
huduma ya uuzwaji wa Fomu kwa ajili ya Viwanja, pia wanatarajia kuanza
kuuza kwa umaa na taasisi mbali mbali miradi mipya ikiwemo wa Tundwi
Songai – Kigamboni jijini Dar es Salaam na ule wa Kingorwila, Morogoro.
Aidha
Bi. Kilave alitumia wito huo kuhamasisha wananchi kujitokeza kwa wingi
ndani ya banda hilo kujipatia elimu mbali mbali zitolewazo na taasisi
hiyo hapa nchini.
Toka
kuanzishwa kwake Taasisi ya UTT-PID imejikita sana katika upimaji wa
maeneno katika mikoa mbalimbali kwa kushirikiana na Halmashauri tofauti
nchini. Miradi mikubwa kama ya Bukoba ambapo viwanja zaidi ya 5,000
vilipima kuuzwa, Halmashauri ya Sengerema kwa ushirikiano na Taasisi
ilipima zaidi ya viwanja 1,200 na uuzaji pamoja na uwekezaji katika
Miundombinu husika unaendelea kwa kasi. Pia Taasisi imewekeza katika
miradi binafsi kama vile eneo la Mapinga katika wilaya ya Bagamoyo huku
ikatarajia uwekezaji mkubwa zaidi katika mikoa ya Morogoro , Arusha, Dar
es Salaam, Maswa, Pwani, Maswa na Ruvuma.
|
No comments:
Post a Comment