Wadhamini
Wakuu wa Ligi kuu ya Vodacom Tanzania bara,Kampuni ya mawasiliano ya
simu Vodacom Tanzania, wamekabidhi kitita cha Shilingi milioni moja
kiungo wa Yanga, Thaban
Kamusoko baada ya kuibuka Mchezaji bora wa ligi hiyo kwa mwezi Desemba
mwaka jana.
Mzimbabwe huyo alikabidhiwa kitita hicho jana na Mtendaji wa Bodi ya
Ligi, Joel Balisidya wakati timu hiyo ikifanya mazoezi Uwanja wa Taifa,
Dar es Salaam kujiandaa na mechi yao ya leo dhidi ya APR ya Rwanda
katika michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika.
Katika kinyang’anyiro cha kuwania tuzo hiyo Kamusoko alimshinda mchezaji
mwenzake wa Yanga, mshambuliaji Amiss Tambwe, raia wa Burundi.
Kamusoko aliisadia timu yake ya Yanga kupata ushindi katika michezo
iliyochezwa mwezi Desemba kwa kushiriki dakika zote katika mechi tatu
zilizochezwa mwezi huo.
Akizungumza baada ya kukabidhiwa kitita hicho wakati mahojiano
aliyofanya na Vodacom Tanzania, Kamusoko aliishukuru kampuni hiyo kwa
kudhamini Ligi Kuu hiyo akisema kwamba imemuwezesha kuonesha kipaji
chake.
Mbali na kuishukuru kampuni hiyo, Kamusoko pa aliwashukuru mashabiki
wa timu yake kwa kuendelea kuwasapoti wachezaji na amesema anawapenda
na anawaamini sana.
"Ninaimani kila timu inapocheza na Yanga inatamani kutufunga, hivyo
ninawaomba mashabiki wawe wavumilivu, lakini tunawahakikishia ushindi
kila tunapocheza kwenye uwanja huu” alisema Kamusoko.
Naye kocha msaidizi wa Yanga, Juma Mwambusi aliwashukuru Vodacom
akisema kwamba wamemchagua mchezaji ambaye ana vigezo vyote vya kuweza
kuwa mchezaji wa Yanga”
Kwa upande wake Meneja Uhusiano wa Vodacom Tanzania,Matina Nkurlu
amewataka wachezaji wanaoshiriki katika ligi hiyo kujituma ili nao
waweze kujinyakulia kitita kama hicho.
“Sisi kama wadhamini wa ligi hii tunaona fahari mchezaji anapojituma
uwanjani na kuisaidia timu yake,hivyo niwaombe wachezaji wajitume ili
waweze kuzawadiwa,”alisema Nkurlu.
|
No comments:
Post a Comment