KWA MAONI AU USHAURI E-mail: inocomm2014@gmail.com, PIGA SIMU: 0714555668

www.utt-pid.org


TEMBELEA: www.utt-pid.org

April 27, 2016

BOBAN, TEMI NJE CITY IKIIVAA MTIBWA J’MOSI

Kinnah Phiri 22
Kocha mkuu wa Mbeya City fc Kinnah Phiri ametangaza orodha ya nyota 18 watakao kuwa sehemu ya mchezo wa ligi kuu ya Vodacom Tanzania bara dhidi ya Mtibwa Sugar, mchezo  uliopangwa  kuchezwa jumamosi hii  Manungu Complex , Turiani, Morogoro.
Akizungunza na Mbeya City Fc muda mfupi  baada ya kumalizika kwa mazoezi ya asubuhi kwenye uwanja wa Sokoine jijini hapa, Kocha Phiri alisema kuwa hana tatizo na nafasi  ya 10 iliyopo timu yake hivi sasa kwenye msimamo wa ligi kwa sababu anaamini ushindi kwenye michezo miwili ijayo utakifanya kikosi chake kusogea mpaka nafasi ya 8.
“Msimamo wa ligi unaonyesha tuko kwenye nafasi ya 10, hili siyo tatizo sana kwa sababu kushinda mechi mbili zijazo kutatuingiza kwenye timu nane bora, hili ndiyo lengo letu, tunayo  michezo minne mbele nina uhakika kwamba kila mchezaji anafahamu kuwa tunatakiwa kuongeza pointi zaidi ili tumelize ligi tukiwa sehemu ya timu nane za juu” alisema. 
Akiendelea zaidi Kocha  Phiri alisema kuwa kwenye mchezo huo wa  morogoro kikosini atawakosa nyota kama Raphael Daud anayeguza majereha ya mguu pia mlinzi Haruna Shamte  aliyekwenye zuio la kucheza kufuatia kadi za njano, huku pia akiwakosa Haruna Moshi Boban na nahodha Temi Felix ambaye  kwa muda mrefu amekuwa nje ya kikosi kutokana na matatizo ya kifamilia.
“Ni wazi hatutakuwa na Haruna Moshi Boban anayesumbuliwa na maralia, pia tunamkosa Temi, tunafahamu alikuwa nje ya timu  akishughulikia masuala ya kifamilia amerudi kambini juzi hivyo kwa vyovyote hawezikuwa sehemu ya mchezo huo, Rahael Daud ni mgonjwa na Haruna Shamte ana  zuio la kadi za njano, kutokuwepo kwao hakuondoi dhamira yetu ya kushinda mchezo kwa sababu tumekuwa namaandalizi mazuri na muhimu kwa wachezaji wetu wengine ambao sasa wako tayari” …  alimaliza Kocha Phiri na kutaja baadhi ya nyota wakaosafiri tayari kwa kuivaa Mtibwa Sugar jumamosi hii.

No comments:

Post a Comment