Naibu
Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dk Hamisi
Kigwangalla ametoa siku 60 kwa uongozi wa Hospitali ya Wilaya ya
Korogwe, Magunga, kurekebisha miundombinu ya majitaka hususan wodi ya
wazazi na chumba cha upasuaji.
Alitoa agizo hilo juzi baada ya kukagua shughuli za utaoji huduma, ikiwamo kushuhudia changamoto zinazowakabili.
Dk
Kigwangalla alikumbana na changamoto ya uchakavu wa miundombinu ya
majitaka, ambayo imekuwa kikwazo kwa utendaji wa watumishi na wagonjwa.
“Mfumo
wa majitaka hapa hauko vizuri, ni hatari kwa afya zenu watumishi na
wagonjwa, nawapeni siku 60 kuhakikisha mmefanyia marekebisho,” aliagiza.
Mganga
Mfawidhi wa Hospitali hiyo, Dk Gwamaka Mwabulambo alimweleza Naibu
Waziri huyo kwamba mwaka wa fedha wa 2016/17, zimetengwa Sh50 milioni
kwa ajili ya ukarabati wa hospitali.
Mkuu
wa Wilaya ya Korogwe, Hafsa Mtasiwa alisema agizo hilo limetolewa
wakati mwafaka kwani litasaidia kunusuru milipuko ya magonjwa ya
kuambukiza na aliahidi kulisimamia.
No comments:
Post a Comment