Vijana
watano kutoka Tanzania ni miongoni mwa vijana 30 wanaoshiriki katika
mafunzo ya wawezeshaji wa ujasiliamali unaozingatia mazingira
yanayofanyika jijini Beja, nchini Ureno.
Mafunzo
hao ambayo yanafanyika kwa muda wa siku saba yanalenga kuwajengea uwezo
vijana hao kuendesha mafunzo kwa vijana wenzao katika nchi wanakotoka
ili kusaidia kupunguza tatizo la ajira na uharibifu wa mazingira.
Nchi
zinazoshiriki mafunzo hayo na majina ya taasisi zinazoshiriki kwenye
mabano ni pamoja na wenyeji Ureno (Check In), Italia (Cesie), Argentina
(Subiral Sur), Slovenia (Pina), Nepal (CNN) na Tanzania (TYCEN) ambapo
kila nchini imewakilishwa na vijana watano chini ya mradi wa
ujasiliamali wa kujali mazingira ‘Green Entrepreneurship’.
Washiriki
wakiwa katika picha ya pamoja walipotembelea kiwanda cha kuchakata taka
cha Resialentejo, wakiongozwa na Injinia wa kiwanda hicho Pedro Sobral.
Washiriki
wakiwa katika picha ya pamoja walipotembelea Halimashauri ya Manispaa
ya Jiji la Beja ambao walipokelewa na Sonia Calvario Mshauri wa Meya wa
Manispaa hiyo.
Mkurugenzi wa TYCEN, Chris Ndalo kutoka Tanzania akitoa mada wakati mafunzo hayo.
Mmoja wa wawezeshaji katika mafunzo hayo, Olga Kuczynska.
No comments:
Post a Comment