KWA MAONI AU USHAURI E-mail: inocomm2014@gmail.com, PIGA SIMU: 0714555668

www.utt-pid.org


TEMBELEA: www.utt-pid.org

April 27, 2016

RAIS MAGUFULI AUNGANA NA RAIS KENYATTA WA KENYA KUOMBOLEZA KIFO CHA MKE WA RAIS MSTAAFU MAMA LUCY KIBAKI

Marehemu Lucy Kibaki akiwa na Mumewe Rais Mstaafu wa Kenya Mzee Mwai Kibaki siku ya ndoa yao mwaka 1962.
 ********
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe  Magufuli  amemtumia salamu za rambirambi Rais wa Jamhuri ya Kenya mheshimiwa Uhuru Kenyatta,kufuatia kifo cha mke wa Rais  Mstaafu wa Kenya mama Lucy  Kibaki aliyefariki dunia leo tarehe 26 April 2016

Mama Lucy Kibaki ambaye ni mke wa Rais Mstaafu wa Kenya Mheshimiwa Mwai Kibaki amefariki dunia jijini London nchini uingereza ambako alikuwa akipatiwa matibabu.

Katika salamu hizo,Rais Magufuli ameeleza kushtushwa na kifo hicho na kuongeza kuwa Kenya imempoteza mtu mhimu aliyetoa mchango mkubwa katika maendeleo ya nchi yake.

"Kupitia kwako Rais wa Jamhuri ya Kenya mheshimiwa Uhuru Kenyatta napenda kumpa pole nyingi  Rais Mstaafu wa Kenya Mheshimiwa Mwai Kibaki,Familia yake,ndugu,jamaa na marafiki wote walioguswa na msiba huu mkubwa." Amesema Rais Magufuli.

Dkt  John  Pombe Magufuli pia amemuombea marehemu Lucy Kibaki apumzishwe mahali pema peponi,Amina.

No comments:

Post a Comment