KWA MAONI AU USHAURI E-mail: inocomm2014@gmail.com, PIGA SIMU: 0714555668

www.utt-pid.org


TEMBELEA: www.utt-pid.org

April 5, 2016

RC MPYA WA MKOA WA DAR ES SALAAM MH.PAUL MAKONDA AKABIDHIWA OFISI

Aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Said Sadiki akisaini hati ya makabidhiano. Kushoto ni Mkuu mpya wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda.
Aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Said Sadiki akisaini hati ya makabidhiano. Kushoto ni Katibu Tawala Mkoa wa Dar es Salaam, Theresia Mmbando na katikati ni Mkuu mpya wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda.
Aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Said Sadiki akimkabidhi vitendea kazi vyote Mkuu mpya wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda, wakati alipomkabidhi ofisi jijini hivi karibuni.
Mkuu mpya wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda, akizungumza wakati akitoa shukurani zake na kuelezea mwelekeo wake wa kiutendaji kwenye mkoa huo, mara baada ya kukabidhiwa ofisi rasmi na aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Said Sadiki (wapili kushoto), jijini hivi karibuni.
Mkuu mpya wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda, akizungumza mara baada ya kukabidhiwa ofisi rasmi na aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Said Sadiki (katikati), jijini hivi karibuni.
Mkurugenzi Mtendaji wa benki ya DCB, Edmund Mkwawa (kushoto), akimkabidhi mfano wa hundi ya sh. milioni 10, Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda kwa ajili ya kusaidia ujenzi wa Kituo cha Polisi cha Chanika jijini hivi karibuni, wakati alipokabidhiwa ofisi rasmi na aliyekuwa Mkuu wa Mkoa huo, Said Sadiki (hayupo pichani). Wapili kulia ni Kamanda wa Polisi wa Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Kamishna Simon Siro.
Mkuu mpya wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda, akipiga picha ya pamoja na Kamati ya Ulinzi na Usalama ya mkoa. Katikati ni aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Said Sadiki aliyemkabidhi rasmi ofisi hiyo.
Mkuu mpya wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda, akipiga picha ya pamoja na Watendaji wa Mkoa wa Dar es Salaam.
Mkuu mpya wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda, akipiga picha ya pamoja na Watendaji wa Benki ya DCB.
Mkuu mpya wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda, akipiga picha ya pamoja na Waandishi wa habari. Watatu kulia ni Mkurugenzi Mwendeshaji wa blogu hii ya bayana, Kassim Mbarouk.
Mkuu mpya wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda, akipiga picha ya pamoja na Viongozi wa Vyama vya Wafanyakazi wa Mkoa wa Dar es Salaam.

No comments:

Post a Comment