![]() |
Waziri
Mkuu Kassim Majaliwa amewaagiza maofisa biashara wa wilaya, mikoa na
Taifa kukagua maghala yote ya wafanyabiashara walioficha sukari na
kuwachukulia hatua.
Waziri
Majaliwa alisema hayo leo asubuhi wakati akihitimisha mjadala wa hotuba
ya mapato na matumizi ya ofisi yake na kuliomba Bunge likubali
kupitisha.
Waziri Mkuu alisema ni kweli kwamba kuna upungufu wa sukari nchini, ingawa pia upo udanganyifu kwa baadhi ya wafanyabiashara.
Alisema
takwimu kutoka kwa wataalamu zinaeleza kwamba mpaka sasa kuna tani
37,000 za sukari katika maghala nchini, lakini imekuwa haionekani kwa
sababu wafanyabiashara wakubwa wameificha ili waiuze kwa bei kubwa.
|
April 27, 2016
SERIKALI YAKIRI UPUNGUFU WA SUKARI, YAAGIZA NCHI ZA NJE
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment