Mwanzilishi
wa Taasisi ya Mkapa (Mkapa Foundation), Rais Mstaafu wa awamu ya tatu,
Mh. Benjamin William Mkapa (kushoto), mgeni rasmi Rais na Mkurugenzi
Mkuu wa Makampuni ya Mohammed Enterprises Tanzania Limited (MeTL Group),
Mohammed Dewji (kulia) pamoja na Mwenyekiti wa bodi ya wadhamini ya
Mkapa Foundation, Balozi Charles Sanga wakiwasili katika sherehe za
miaka 10 ya Mkapa Foundation zilioambatana na harambe ya kutunisha mfuko
wa taasisi hiyo zilizofanyika kwenye ukumbi wa Golden Jubilee Tower.
(Picha na Zainul Mzige wa Modewjiblog)
…………………………………………………………………………….
Katika
kusherekea miaka 10 tangu kuanzishwa kwa taasisi ya Benjamin Mkapa,
imefanyika harambee ambapo jumla ya Bilioni moja na Milioni mia moja na
sabini zimechangishwa na wadau mbalimbali ambao wanasapoti taasisi hiyo
inayojishughulisha kusaidia jamii.
Baadhi
ya watu ambao wamechangia pesa ni pamoja na Rais na Mkurugenzi Mtendaji
wa Makampuni ya Mohammed Enterprises Tanzania Limeted (METL Group),
Mohammed Dewji ambaye amechangia kiasi cha Milioni 210 akiwa kama mgeni
rasmi katika sherehe za kutimiza miaka 10 tangu kuanzishwa kwa Taasisi
ya Benjamini Mkapa (Mkapa Foundation) ambapo Milioni 200 imetolewa na
Taasisi ya Mohammed Dewji (Mo Dewji Foundation) na Milioni 10 imetolewa
na MeTL Group.
Akitoa
hotuba katika sherehe hiyo, Mohammed Dewji amesema kuwa ametoa msaada
huo ili kuiongezea nguvu Taasisi ya Benjamin Mkapa (Mkapa Foundation)
katika kutoa huduma mbalimbali kwa jamii ya Watanzania.
Alisema
kuna changamoto nyingi nchini ambazo zimekuwa zikijitokeza na ili
kukabiliana nazo zinahitajika taasisi kama ya Benjamin Mkapa ili ziweze
kusaidiana na Serikali na ili waweze kutatua changamoto hizo
zinahitajika sekta binafsi kusaidiana nao kukabili changamoto hizo.
“Nimekuwa
mstari wa mbele kusaidia sehemu ambazo zinaonekana kuwa na mahitaji na
changamoto nchini zipo nyingi haina jinsi inabidi kushirikiana ili
kupambana na changamoto hizo,” alisema Dewji.
Aidha
Rais na Mkurugenzi Mkuu huyo wa MeTL Group aliyataka mashirika binafsi
mengine kuungana kwa pamoja na kusaidia kumaliza changamoto zilizopo
nchini kwani anaamini kuwa wana nafasi kubwa kukabiliana na matatizo
hayo na kuweza kuyamaliza.
Nae
mwanzilishi wa Taasisi ya Mkapa (Mkapa Foundation), Rais Mstaafu wa
awamu ya tatu, Mh. Benjamin William Mkapa alimshukuru Mohammed Dewji kwa
msaada ambao amewapatia na anaamini ni mmoja wa watu wa kuigwa nchini
kutokana na misaada ambayo amekuwa akiitoa nchini kwa kupitia taasisi
yake ya Mohammed Dewji (Mo Dewji Foundation).
“Mohammed
Dewji ni mfano wa kuigwa nchini na ameweza kuboresha biashara ya
Tanzania kimataifa, ninaamini utadumu kwa kipindi kirefu zaidi na kuwa
balozi mzuri wa Tanzania,” alisema Mkapa.
Katika
sherehe hizo za kuadhimisha miaka 10 tangu kuanzishwa kwa Taasisi ya
Benjamin William Mkapa, kulifanyika harambee ambapo jumla ya Bilioni
moja na Milioni mia moja na sabini zilichangishwa.
Afisa
Mtendaji Mkuu wa Benjamin Mkapa Foundation, Dk. Ellen Mkondya Senkoro
akitoa historia fupi ya taasisi hiyo kwa wageni waalikwa katika hafla
hiyo.
Mwenyekiti
wa bodi ya wadhamini ya Mkapa Foundation, Balozi Charles Sanga
akizungumza machache kabla ya kumkaribisha mgeni rasmi kutoa neno katika
sherehe za miaka 10 ya taasisi isiyo ya kiserikali ya Mkapa zilioenda
sambamba na harambe ya kutunisha mfuko huo.
Msaidizi
mwandamizi katika utawala wa Kampuni ya MeTL Group, Shemane Amin pamoja
na Makamu wa Rais wa Makampuni ya MeTL Group, Vipul Kakad wakiwa kwenye
dakika moja ya ukimya kumkumbuka Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage
Nyerere ambapo ilikuwa ni siku yake ya kuzaliwa wakati wa sherehe za
miaka 10 ya Mkapa Foundation zilizoenda sambamba na harambe ya kutunisha
mfuko wa taasisi hiyo zilizofanyika April 13, 2016.
Rais
na Mkurugenzi Mkuu wa Makampuni ya Mohammed Enterprises Tanzania Limited
(MeTL Group), Mohammed Dewji akizungumza kwenye sherehe za miaka 10 ya
Mkapa Foundation zilizoenda sambamba na harambe ya kutunisha mfuko wa
taasisi hiyo zilizofanyika April 13, 2016.
No comments:
Post a Comment