Waziri wa Habari, Utamaduni,
Sanaa na Michezo Mhe. Nape Nnauye akisalimia wananchi wa Mkoa wa Katavi
alipowasili katika mkoa huo jana kukutana na wadau wa sekta
anazozisimamia pamoja na kutoa vitendea kazi kwa maafisa habari wa mkoa
wa Katavi na kutembelea mitambo ya kurushia matangazo ya TBC. Kushoto ni
Mkuu wa wilaya ya Mpanda Mhe. Paza Mwamlima.
Waziri wa Habari, Utamaduni,
Sanaa na Michezo Mhe. Nape Nnauye akizungumza na watendaji wa Mkoa wa
Katavi alipowasili katika ofisi za mkoa huo na badae kukutana na wadau
wa sekta anazozisimamia pamoja na kutoa vitendea kazi kwa maafisa habari
wa mkoa wa Katavi na kutembelea mitambo ya kurushia matangazo ya TBC.
Wadau wa sekta za Habari,
Utamaduni, Sanaa na Michezo Mkoa wa Katavi wakimsikiliza Waziri mwenye
dhamana na sekta hizo Mhe. Nape Nnauye (hayupo pichani) alipofanya kikao
nao jana mkoani hapo na kuahidi kutatua baadhi ya kero zinazowakabili.
Waziri wa Habari, Utamaduni,
Sanaa na Michezo Mhe. Nape Nnauye akikagua iPad kabla ya kumkabidhi Mkuu
wa wilaya ya Mpanda Mhe. Paza Mwamlima iPad nne kwa ajili ya maafisa
habari waliopo katika Mkoa wa Katavi na Wilaya zake jana mkoani Katavi.
Mkuu wa wilaya ya Mpanda Mhe.
Paza Mwamlima akifurahi na kumpa mkono Waziri wa Habari, Utamaduni,
Sanaa na Michezo baada ya kupokea iPad nne kwa ajili ya maafisa habari
waliopo katika Mkoa wa Katavi na Wilaya zake jana mkoani Katavi.
Picha na: Genofeva Matemu – Maelezo, Katavi
…………………………………………………………………………………………….
Na: Genofeva Matemu – Maelezo, Katavi
Tarehe: 05/04/2016
Taasisi za serikali zimetakiwa
kuwashirikisha maafisa habari waliopo katika taasisi zao katika vikao
vya maamuzi ili waweze kua na taarifa na kufahamu maamuzi ya michakato
inayoendelea hivyo kupata nguvu na uelewa mzuri wa kwenda kueleza umma
pale wanapotakiwa kutolea ufafanuzi.
Kauli hiyo imetolewa na Waziri wa
Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Nnauye wakati wa ziara
yake jana katika Mkoa wa Katavi kukutana na wadau wa sekta
anazozisimamia pamoja na kutoa vitendea kazi kwa maafisa habari wa Mkoa
huo na kutembelea mitambo ya kurushia matangazo ya TBC.
Mhe. Nnauye amesema kuwa maafisa
habari katika taasisi za serikali wamekuwa wakinyimwa nguvu ya kushiriki
katika vikao vya taasisi hivyo kushindwa kutolea maamuzi masuala
mbalimbali pale wanapohitajika katika vyombo vya habari.
Aidha Mhe. Nnauye amewataka
waandishi wa habari kufanya kazi kwa kufuata sheria kanuni na taratibu
kwani serikali inawajali na kuwathamini kwa kazi nzuri wanayoifanya ya
kuelimisha jamii.
“Mswada wa sheria ya huduma wa
vyombo vya habari umelinda maslahi ya waandishi wa habari na Sheria hii
imebana vigezo ambapo kama itapita itasaidia kupambana na utitiri wa
vyuo visivyokuwa na sifa pamoja na changamoto zingine zinazoikabili
sekta hii” amesema Mhe. Nnauye.
Aidha Mhe. Nnauye amewaomba watu
wa TCRA kusimamia vizuri maudhui ya Radio na Television kwa kuwa wakali
na kuacha kucheka na watu ambao wanaweza kutumia vibaya mabadiliko ya
sayansi na teknolojia kuwaga jamii yetu kidini, kikabila, kikanda na
rangi kwa kufanya matangazo ya kuligawa taifa letu.
Naye mwandishi wa habari kutoka
Clous FM Bw. Ezron Mahanga ameiomba serikali kuendelea kupambana kulinda
maslahi ya waandishi wa habari kwa kuwasimamia kwa karibu ili wamiliki
wa vyombo vya habari waache kuwatumia kwa maslahi yao binasfi bila
kujali utu wa waandishi wa habari wanaofanya kazi katika mazingira
magumu.
No comments:
Post a Comment