Wizara ya Afya, Maendeleo ya
Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto imesikitishwa na kukemea vikali tukio la
mzazi kumbaka na kumlawiti mtoto wake wa kufikia mwenye umri wa mwaka
mmoja na nusu, kitendo kilichofanywa na John Donald (35) mkazi wa
Kiyangu, Manispaa ya Mikindani mkoani Mtwara.
Tukio hili la kubaka na
kulawitiwa ni ukatili wa hali ya juu dhidi ya mtoto maana husababisha
maumivu makali ikiwa ni pamoja na kumdhuru mtoto kimwili, kisaikolojia,
kijamii na kihisia. Aidha, vitendo hivi, vinaacha kovu la kudumu
kimwilini, kiakili, kimaadili, kijamii, ulemavu, maumivu, na wakati
mwingine husababisha kifo; jambo ambalo linahitaji ulinzi thabiti katika
kuhakikisha watoto wanaishi mazingira salama na rafiki.
Ukatili alilofanyiwa mtoto eneo
la Kinyangu, manispaa ya Mikindani, ni ukiukwaji mkubwa wa haki za mtoto
ambao huchangia kurudisha nyuma ustawi na maendeleo ya Mtoto na ni
kinyume cha Sheria ya Mtoto Na. 21 ya mwaka 2009.
Wizara inatoa pongezi kwa Jeshi
la Polisi mkoani Mtwara kwa kumkamata mtuhumiwa na kumfikisha mahakamani
ili hatua za kisheria zichukuliwe. Vile vile, Wizara inaipongeza
Mahakama ya Wilaya ya Ilala, mkoani Dar es salaam dhidi ya Omary hamisi
(25), mkazi wa Gongo la Mboto, Dar es salaam, ya kutumikia kifungo cha
maisha jela, baada ya kupatikana na hatia ya kumlawiti mtoto wa miaka
tisa mwenye ulemavu wa kusikia na kuongea. Uamuzi huu ni kielelezo kuwa,
wananchi wakitoa ushahidi wa matukio ya ukatili dhidi ya watoto,
watuhumiwa watachukuliwa hatua kali ili kuwa fundisho kwa wananchi
wanaowanyanysa watoto.
Wizara inamwelekeza Afisa Ustawi
wa Jamii na Afisa Maendeleo ya Jamii wa Mkoa wa Mtwara kuwasiliana na
wadau wengine katika ngazi zote kuhakikisha mama na mtoto wanapata
huduma ya afya na ushauri na kufuatilia mwenendo wa shauri hili.
Imetolewa na
Erasto Ching’oro
Msemaji wa Wizara
Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto
No comments:
Post a Comment