Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Mhe. Zelote Stephen (kulia) pamoja na Mkuu wa Wilaya ya Sumbawanga Mhe. Mathew Sedoyeka (kushoto) wakiteta jambo na Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Nnauye baada ya kuwasili katika Mkoa wa Rukwa jana kuzungumza na wadau wa sekta anazosimamia.
Waziri wa Habari, Utamaduni,
Sanaa na Michezo Mhe. Nape Nnauye akizungumza na viongozi wa CCM Mkoa wa
Rukwa jana wakati wa ziara yake mkoani humo kukutana na wadau wa sekta
anazozisimamia. Kushoto kwa Waziri ni Mwenyekiti wa CCM Rukwa Bw.
Hypolitus Matete
Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Mhe. Zelote
Stephen (kushoto) akuzungumza na Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na
Michezo Mhe. Nape Nnauye alipofika ofisini kwake wakati wa ziara ya
kukutana na wadau wa sekta ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo pamoja
na kutoa vitendea kazi kwa maafisa mawasiliano jana Mkoani Rukwa.
Waziri wa Habari, Utamaduni,
Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye akizugumza na watendaji kutoka
Mkoa wa Rukwa pamoja na wadau wa kada za Habari, Utamaduni, Sanaa na
Michezo alipokutana nao jana Mkoani hapo kujadili mambo mbalimbali
katika sekta hizo pamoja na kutoa vitendea kazi kwa maafisa mawasiliano.
Baadhi ya watendaji kutoka Mkoa
wa Rukwa pamoja na wadau wa kada za Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo
wakimsikiliza kwa makini Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo
Mhe. Nape Moses Nnauye (hayupo pichani) alipofanya ziara yake jana
Mkoani Rukwa kujadili mambo mbalimbali pamoja na kukagua ofisi za TBC
na kutoa vitendea kazi kwa Maafisa Mawasiliano wa Mkoa wa Rukwa.
Waziri wa Habari, Utamaduni,
Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye akiikagua iPad kabla ya
kumkabidhi Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Mhe. Zelote Stephen (kushoto) kwa ajili
ya kuboresha utendaji kazi kwa maafisa mawasiliano waliopo Mkoani hapo.
Mhe. Nnauye alikabidhi iPad tatu kwa Mkoa wa Rukwa jana baada ya
kufanya ziara fupi na kuonana na wadau wa sekta anazozisimamia
Mkuu wa Wilaya ya Nkasi Mhe. Iddi
Kimanta akitoa taarifa fupi kuhusu sekta za Habari, Utamaduni, Sanaa na
Michezo kwa Waziri wa sekta hizo Mhe. Nape Moses Nnauye alipofanya
ziara Wilayani hapo jana Mkoani Rukwa.
Waziri wa Habari, Utamaduni,
Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye akizungumza moja kwa moja
kupitia radio ya Wilaya NKasi FM alipofanya ziara katika radio hiyo
kuona mafanikio yaliyoletwa na Wilaya ya Nkasi kwa kuwa na radio ya
Wilaya.
Picha na: Genofeva Matemu- Maelezo, Rukwa
No comments:
Post a Comment